Picha Zilizopigwa Angani Zaonyesha Madhari Nzuri ya Cambodia

Cambodian countryside

Sehemu ya kijijini nchini Cambodia

Wakati akipiga picha za dokumentari nchini Cambodia, mtayarishaji wa filamu Roberto Serrini alipata wasaa wa kutembelea vijiji kadhaa vya mjini na vijijini katika nchi hiyo. Timu yake ilitumia ndege aina ya DJI Phantom na kamera ya GoPro kupata picha za uzuri halisi wa Cambodia. Alielezea zoezi hilo la upigaji picha kama ‘uzoefu wa mzuri ajabu':

Kwenye eneo la Phnom Pehn na kwenye kijiji cha Anluk Leak, niliweza kuchnguza uzuri wa kifilamu wa nchi hii nzuri kutoka angani.

Uzoefu mzuri ajabu sana, kwa sababu wengi wa watoto hawa hawjawahi kuona televisheni, achilia mbali ndege inayopaa angani; mchanganyiko wa mvuto, msisimko na maajabu ya wanachokiona ndilo lilikuwa likionekana kwenye nyuso zao.

http://vimeo.com/serrini/aerialcambodia

Hapa chini ni baadhi ya picha za kwenye mtandao wa Flickr zinazoelezea safari ya Roberto nchini Cambodia:

Mwonekano wa kijiji kimoja wapo nchini Cambodia

Hekalu jijini Phnom Penh, mji mkuu wa Cambodia

Mtawa akitembea kwenye jengo la umma nchini Cambodia

Usafiri maarufu wa Cambodia uitwao tuktuk

Hekalu jijini Phnom Penh

Pikipiki ya matairi matatu maarufu kama tuktuk ambayo ni usafiri maarufu wa umma nchini Cambodia

*Video na picha za Roberto Serrini, zimetumiwa kwa ruhusa yake.

Exit mobile version