Portland, kampuni yenye makazi yake jijini London ikishughulika na mawasiliano, imechambua twiti zipatazo bilioni 1.6 kwa kuzingatia maeneo na alama ishara (hashtag) zipatazo 5,000 barani Afrika kwa ajili ya ripoti ya tatu ya “Afrika Ilivyotwiti“.
Ripoti hiyo ina mada 12 zinazogusa namna gani mtandao wa twita unavyohusiana na masuala kama ugaidi barani Afrika, hatua za kukabiliana na Ebola, na maendeleo ya kiuchumi barani humo.
Kampuni hiyo ilitumia nyenzo maalumu ya kuchambua mitandao ya kijamii iitwayo Sysomos ili kukusanya na kuchambua alama ishara zipatazo 5,000. Hata hivyo, haikuweza kukusanya taarifa za Sudani Kusini na Jamhuri ya Kongo kwa sababu ya kukosekana kwa takwimu zake kwenye mitandao ya kijamii.
“Tafiti zetu zilizopita zilionesha kwamba mtandao wa Twita barani Afrika ulikuwa ni kama uwanja wa watu kukutana au kufanyia mazungumzo ya utani. Utafiti huu umeonesha kwamba jukwaa hili linazidi kuwa maarufu likisheheni mijadala makini inayohusu siasa na serikali,” Mark Flanagan, Mkuu wa Maudhui na Mikakati ya Kidijitali ananukuliwa katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Mambo Muhimu Yaliyojitokeza:
Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa twita wamekuwa wakijadili matokeo hayo kwenye mtandao wa Twita kwa kutumia alama ishara ya #HowAfricaTweets [AfrikaInavyoTwiti].
First cases of #Ebola were being discussed on social media before any official announcement was made by WHO or others.” #HowAfricaTweets
— Rosebell Kagumire (@RosebellK) April 7, 2016
Matukio ya mwanzo ya Ebola yalijadiliwa kwenye mitandao ya kijamii kabla ya tangazo rasmi kutolewa na Shirika la Afya Duniani [WHO] na wengineo.
Africans were especially vocal on a handful of international events on Twitter incl Islamic State, #BlackLivesMatter – #HowAfricaTweets
— Rosebell Kagumire (@RosebellK) April 7, 2016
Waafrika walipaza sauti kwenye matukio machache ya kimataifa kwenye mtandao wa twita ikiwa ni pamoja na kikundi cha Kigaidi cha Dola ya Kiislam [ISIS]
“Gabon is a French-speaking country in central Africa, but three of its top ten tweets had to do with events in Nigeria” #HowAfricaTweets
— Djelissah (@Melsse) April 7, 2016
Gabon ni nchi inayotumia Kifaransa Afrika ya Kati, lakini twiti zake tatu maarufu zilihusiana na matukio ya Naijeria
#AfrikaInavyoTwiti
Alama Ishara tano maarufu kutoka Uganda
1. #Uganda
2. #UgandaDecides [UgandaYaamua]
3. #News [Habari]
4. #Latest [Habari Mpya]
5. #MUFC— Pru Nyamishana (@nyapru1) April 6, 2016
#AfrikaInavyoTwiti
Alama Ishara tano maarufu kutoka Uganda
1. #Uganda
2. #UgandaYaamua
3. #Habari
4. #HabariMpya
5. #MUFC
The small island of Comoros had the highest level of Tweets Per Capita of 0.77 across the continent. #howafricatweets
— Grace Natabaalo (@Natabaalo) April 6, 2016
Kisiwa kidogo cha Komoro kilikuwa na kiwango cha juu cha twiti kinachofikia twiti 0.77 kwa kila mtu
Ripoti hiyo, kwa ujumla, imepokewa kwa maoni chanya. Hata hivyo, Mwesigwa Daniel, mwandishi wa True Africa alitwiti:
The #HowAfricaTweets report is another a piece of cheap popularity. So much left out.
— Mwesigwa Daniel (@valanchee) April 7, 2016
Ripoti hii nayo ni namna nyingine ya kutafuta umaarufu wa haraka. Mengi yameachwa.
Akijibu twiti ya Reed Kramer, Demba Kandeh, mwandishiwa Global Voices, alikuwa na haya ya kusema:
@reedkramer @PortlandComms @twitter interesting findings; sounds like comparing apples n oranges, #AfricaIsNotACountry #HowAfricaTweets
— Demba Kandeh (@saadems) April 7, 2016
Matokeo yanayofikirisha; inaonekana kama kulinganisha maembe na machungwa, #AfrikaSioNchi