Jamii ya Lumad Nchini Ufilipino Yasimama Kidete dhidi ya Uonevu

Lumad leaders display banner calling for the protection of their communities as they march towards Manila. Photo from the Facebook page of ST Exposure

Viongozi wa Lumad wakionesha bango linaloshinikiza kulindwa kwa jamii yao walipokuwa katika matembezi ya kuelekea jijini Manila. PIcha kutoka Ukurasa wa Facebook wa ST Exposure

Mnamo Oktoba, 2015, zaidi ya watu 700 wa jamii ya Lumad (Raia wazawa kutoka katika kisiwa cha Mindanao kilichopo kusini mwa nchi ya Ufilipino) walisafiri maelfu ya kilomita ikiwa ni pamoja na kuweka kambi katika jiji la manila kwa lengo la kushinikiza kuondolewa kwa wanajeshi pamoja na kusitisha matumizi ya nguvu za kijeshi katika jamii zao.

Ukijulikana kama Manilakbayan 2015, msafara wa watu ambao pia una lengo la kutafuta kuungwa mkono na jamii ya kimataifa katika kukomesha ukiukwaji wa haki za bianadamu unaofanywa na majeshi ya nchi dhidi ya jamii ya Lumad.

Shuhuda kutoka kwa baadhi ya jamii ya watu wa Lumad zilisambazwa kupia mtandao wa Facebook na kikundi cha Southern Tagalog Exposure.

Kiungo habari #StopLumadKillings kilipata umaarufu nchini Ufilipino mara baada ya kutokea kwa mauaji ya kutisha ya Emerito Samarca ambaye ni mkuu wa shule ya jamii ya watu wa Lumad pamoja na mauaji ya raia wazawa Dionel Campos na Bello Sinzo, mauaji yaliyotokea mwezi Septemba 1, 2015.

Hili ni moja ya tukio la aina yake ambalo wanaharakati wanaliona kuwa ni kampeni ya kimkakati ya ukandamizaji dhidi ya raia wazawa wa Mindanao, ikies ni pamoja na kuwalenga viongozi wao na kuwaua, ufungaji wa shule za raia wazawa, pamoja na ardhi yao kukaliwa na wanajeshi.

Mashirika ya Lumad yanaelezea kuwa yanalengwa chini ya mwavuli wa organizations explain that they are being targeted at the behest of Uchimbaji madini mkubwa, mashamba makubwa ya kilimo, pamoja na makampuni mengine yaliyo na uchu wa wa ardhi yenye rutuba ya jamii ya watu wa Lumad.

Majeshi ya Ufilipino yanatuhumiwa pia kwa kuweka wanajeshi na kutoa mafunzo ya kijeshi kwa watu wa jamii ya Lumad kwa ajili ya kukabiliana na ndugu zao wenyewe. Utoaji wa mafunzo ya kijeshi kwa baadhi ya jamii ya watu wazawa imepelekea kuhama kwa maelfu ya watu wa Lumad kutoka Mindanao.

Taarifa hizi fupi zilizokusanywa na Southern Tagalog Exposure yatoa ushuhuda kuhusiana na utoaji wa mafunzo ya kijaeshi kwa jamii ya wazawa pamoja na uporaji wa ardhi za urithi za wazawa.

“Ardhi zetu za urithi zinachukuliwa kwa nguvu. Tunahitaji kuwaondosha wanajaeshi na kuharibu kabisa makundi ya watu waliopokea mafunzo ya kijeshi na ambao ndio wanatuvunjia heshima jamii ya Lumad. Tunahitaji kuishi kwa amani.”
Bai Bibiaon Ligkaian Bigkal, Mwanamke mpambanaji wa Tala-ingod, Davao del Norte

“Wanajeshi wameangamiza kabila letu. Serikali pamoja na mashirika yameweka mbele maslahi yao pekee, na siyo maslahi ya jamii nzima. Watu siyo wa muhimu kwao. Tunapojaribu kulinda aridhi zetu za urithi pamoja na na utamaduni wetu, wanatutuhumu kuwa sisi ni sehemu ya [kundi la waasi], yaani jeshi jipya la watu kama namna ya kuhalalisha kuwaondosha watu kutoka katika makazi yao au kutekeleza mauaji.”
Kaylo, Manobo wa Talaingod, Davao del Norte

“Kutokana na uonevu wa wanajeshi, tulilazimika kuondoka na kuiacha ardhi yetu. Kuachwa bila makazi ni kugumu sana, kukiwana joto kali na bila ya maji. Tunahitaji kurudi kwenye maeneo yetu. Tokea nikiwa mdogo, mimi kama raia wa Lumad niliapa kuendelea kudai haki yetu hadi siku nitakayokufa.”
Krstina Lantao, Eneo la Kusini mwa Mindanao

“Jeshi la Ufilipino liliharibu shule yetu. Pia, lilichoma majengo ya ushirika wetu wa kilimo. Nilijikuta nimefungwa gerezani na sasa nimeshitakiwa kwa kusingiziwa kosa la utekaji. Tuna hamu ya kuipata tena ardhi yetu tuliyoirithi kwa mababu zetu. Popote tutakapokuwa, tutaipigania. Huku ndipo tunapoishi na tulipokulia. Kama tutaporwa ardhi yetu, utamaduni wetu utapotea sambamba na kizazi kijacho.”
Datu Isidro, Kitaotao, Bukidnon

“Chopa ya wanajeshi iliwasili katika makazi yetu. Walichoma nyumba yetu. tulibakiwa tu na nguo tulizokuwa tumevaa. wanajeshi walidai kuwa, watu jamii ya Lumad hawapaswi kwenda shule. Nikiwa mkubwa, nitapenda kuwa mwalimu ili kuwaonesha kuwa mawazo yao siyo sahihi. .”
Kimkim Baliti, 13-year-old Manobo, Talaingod, Davao del Norte

“”Hatutafia kwenye mapambano, bali tutafia kwenye mashimo ya wazi ya uchimbaji madini. Sisi ndio tunaopaswa kunufaika na utajiri wa Mindanao.Wanajeshi wanatutuhumu kuwa sisi ni [kundi la waasi], yaani jeshi jipya la watu kama namna ya kuhalalisha kuwaondosha watu kutoka katika makazi yao au kutekeleza mauaji. Wao ndio wanaopaswa kuondoka kwa kuwa wao ndio wavamizi wa ardhi yetu ya tokea enzi za mababu.”
Jean Derong, Manobo, Davao Oriental

“Jukumu la wanawake katika harakati za kuilinda jamii halisi ya Lumad ni la muhimu. Heshima iliyopo miongoni mwetu ni ya hali ya juu sana. Kwa pamoja, tunahitaji kulinda haki zetu pamoja na ardhi yetu tuliyoirithi kutoka kwa mababu zetu.”
Bai Aida Seiza, Manobo, Paquibato, Davao City

Exit mobile version