Wanaharakati Waomba Ulinzi kwa Makabila Yanayopinga Uchimbaji Madini Nchini Ufilipino

"Oplan Bayanihan [a military counterinsurgency program] lalazimisha jamii ya Lumadi kuziacha radhi zao, lakini pia wanaweka mazingira ya makampuni kumiliki ardhi na pia wanatumia majeshi ya Ufilipino kama ulinzi wao huku wakipora na kujizolea maliasili ya madini. to evacuate their lands, but also paves the way for corporations to take hold of the land, and use the Armed Forces of the Philippines as their own security force as they plunder and suck the Earth of it's natural elements." Picha na Anakbayan USA.

“Oplan Bayanihan [programu ya kijeshi dhidi ya uhaini] yapelekea jamii ya Lumad kuziacha ardhi zao, lakini pia wanaweka mazingira ya makampuni kumiliki ardhi na pia wanatumia majeshi ya Ufilipino kama ulinzi wao huku wakipora na kujizolea maliasili ya madini.”Picha kwa hisani ya Anakbayan USA.

Akizungumizia habari kuwa shughuli zifananazo za kijeshi pamoja na zile za uchimbaji madini zinachochea kuondosha makabila ya Lumad kwenye maeneo yao, raia wengi wa Ufilipino wameita sserikali kuchukua hatua mapema iwezekanavyo ili kukomesha ukatili dhidi ya wazawa. Lumad ni neno linalotumika kutambulisha makabila ya wazawa wa Mindanao, kisiwa cha pili kwa ukubwa nchini Ufilipino kilichopo upande wa kusini wa nchi hii.

Viongozi wa Lumad kutoka kwenye jimbo la Surigao walitaarifu kuwa vikundi vya wanamgambo vilivamia shule zao pamoja na wanajamii, hali iliyolazimu zaidi ya watu 2,000 kuyakimbia makazi yao maeneo ya milimani na kutafuta hifadhi katika maeneo ya jiji. Wengi wao walikuwa watu wa jamii ya Lumad ambao walipinga vikali uvamizi wa makampuni ya uchimbaji madini.

Tume ya Taifa ya Utamaduni na Sanaa (NCCA), moja ya taasisi za serikali, ilielezea kuwa, ukatili dhidi ya Lumad kuwa ni shambulio dhidi ya utamaduni wa Kifilipino:

Tume ya Taifa ya Utamaduni na Sanaa (NCCA) inawatambua raia hawa wazawapamoja na viongozi wao kama kiini na tegemeo la urithi wa kiutamaduni wa nchi ya Ufilipino. Uvamizi huu ni kikwazo dhidi ya utamaduni wetu wa kipekee wa kisanaa. Ukatili wao ni ukatili dhidi ya utu wa watu wetu. Kama watoa elimu wa kipindi kirefu, maarifa na utendaji, kuwajeruhi ni kuharibu msingi wa utamaduni ambao ndio tegemeo la maendeleo endelevu ya nchi yetu.

Kwa siku kadhaa za mwezi Septemba, kiungo habari cha Twitter#StopLumadKillings‬‬ kilipata umaarufu miongoni mwa raia wa mtandaoni wa nchini Ufilipino pale walipotumia mitandao ya kijamii kama namna ya kuwaunga mkono watu wa jamii ya Lumad waliofukuzwa kwenye makazi yao. Zifuatazo ni baadhi ya picha na jumbe zikionesha kuiunga mkono jamii ya Lumad:

Tangazo likionesha kusisitiza msimamo wa Kanisa Katoliki katika Jiji la Tandag ambapo zaidi ya watu wa jamii ya Lumad 2,000 walioyakimbia makazi yao walipatiwa hifadhi. Picha iliwekwa kwenye mtandao wa Facebook na Manassas Benedict L. Serrano.

Walimu katika jiji la Manila nao wajiunga na kampeni ya kutaka kulindwa kwa jamii ya watu wa Lumad. Picha kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Carl Marc Ramota.

Wanaharakati wanawake jijini Manila waungana kuitetea jamii ya Lumad. Picha kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Tudla

Watumiaji wa Facebook waliombwa kusambaza picha hii ya umbo iliyoasisiwa na makundi ya watetezi wa haki za binadamu kama namna ya kuitetea jamii ya watu wa lumad.

Kmpeni ya #StopLumadKillings imeungwa mkono PI na nchi nyingine. Zifuatazo ni picha zinazoonesha mshikamano wa kimataifa uungaji mkono jamii ya Lamad:

Walimu wa Kifilipino wa Chuo kiuu cha California Berkeley wajitokeza kuiunga mkono jamii ya Lumad. Picha kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Joi Barrios-Leblanc

Wanaharakati wa Kilipino katika Jiji la New York wajitokeza kuiunga mkono jamii ya Lumad. Picha na Anakbayan USA

Familia moja ya Kipalestina pia iliunga mkono kampeni hii. Picha iliwekwa kwenye ukurasa wa Facebook na Mark Moreno Pascual

Wanaharakati wa Ubelgiji waiunga mkono jamii ya Lumad. Picha kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Tinay Palabay

Wanaharakati wanaohudhuria kongamano la nchini ujerumani waunga mkono jamii za Lumad. Picha kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Tinay Palabay

Wanaharakati nchini Uholanzi waiunga mkono jamii ya Lumad. Picha kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Marlon Toledo Lacsamana

‪Muwakilishi maalum wa umoja wa Maifa wa kuratibu haki za raia wazawa, Victoria Tauli-Corpuz, na mtetezi wa haki za binadamu, Michel Forst walilitaka jeshi kuacha kuzishikilia baadhi ya shule za kiutamaduni:‬

Hali ya majeshi kushikilia taasisi za kiraia pamoja na kuwaua raia, hususani maeneo kama shule ambazo zilipaswa kuwa sehemu salama kwa ajili ya watoto wa maeneo haya yaliyo na machafuko, ni mambo yasiyokubalika, wala kuvumilika na ni kinyume kabisa na haki za kimataifa za binadamu na pia ni kinyume na viwango vya kimataifa vya utoaji huduma za kijamii

Hata hivyo, jeshi limekanusha kuwa liliratibu makundi mithili ya jeshi kwa ajili ya kuzidhalilisha jamii za watu wa Lumad. Jeshi lilisisitiza kuwa, vita vya kimakabila ndivyo vilivyokuwa chanzo cha machafuko katika maeneo ya Lumad. Lakini, Gavana wa jimbo alitupilia mbali madai haya na kulitupia jeshi lawama kwa kuasisi na kutoa silaha kwa makundi haya mithili ya jeshi. Seneta wa Ufilipino ameahidi kulifanyia uchunguzi suala hili.

Exit mobile version