Blogu ya Baraza ilichapicha maudhui ya makubaliano hayo ambayo Zambia na Tanzania imeyaleta pamoja na pendekezo la Kenya la kuupinga. Maina anaelezea kwenye Baraza
Kwa upande mmoja ni ukanda wa nchi zinazopinga biashara ukijumuisha Kongo, Ghana, Kenya, Liberia, Mali na Sierra Leone. Kwa upande mwingine, kila mmoja ikiwa na pendekezo lake ni Zambia na Tanzania, ambazo zinataka kuruhusiwa kuuza hifadhi ya pembe za ndovu zilizonazo kwa mkutano ujao wa Doha Machi 13-25 –mkutano wa 15 wa CITES. Pande zote zimetuma mapendekezo kwa sekretarieti ya CITES ba sekretarieti imekuwa na uungwana kwa kuweka mapendekezo hayo kwenye wavuti yao.
Katika posti nyingine kwenye blogu hiyo ya Baraza, Paula anaandika kuhusu kusudio la Uingereza la kupiga kura ya kupinga mapendekezo yote mawili:
Uingereza imesema hapana kwa uuzaji wa pembe za ndovu. Waziri wa Mazingira Hillary Benn alisema usiku wa jana: “Katika mkutano wa CITES mwezi Machi, Uingereza itapiga kura kupinga mapendekezo hayo kutokaTanzania na Zambia ya kuuza pembe za ndovu, na tutazitaka nchi nyingine kupiga kura ya kupinga uuzaji huo.
Paula anaandika kwenye blogu mpya ya WildlifeDirect iitwayo Ban Ivory -inayojitoa mahususi kupiga kampeni kupinga pembe za ndovu- akiuliza “Je, tembo wanathamani kuliko meno yao?”. Anauliza: “Je, tembo ni chanzo tu cha bidhaa ya thamani, pembe zake? Au, je, tembo wanastahili kutendewa kwa upekee?”
Paula anasema kwamba pamoja na kuungwa mkono ambako Waafrika wanakutegemea kutoka nje, vita kwa ajili ya tembo itabidi ianze na Waafrika wenyewe. Anasema:
Mwisho wa siku maandamano upinzani dhidi ya biashara ya pembe za ndovu itabidi uongozwe na Waafrika ikiwa ulimwengu uliobaki utatakiwa kuona kile kinachoifanya kampeni ya Kenya kuwa na nguvu. Lakini ikiwa Wachina na Waasia wengine wataendelea kuwa masoko ya pembe za ndovu na kukataa kufanyia kazi makubaliano ya ndani, katazo hili jipya kwa biashara ya pembe litashindwa na tutaendelea kupoteza tembo.
Kikundi kinachojulikana kama Jukwaa la Ndovu Kenya kinaongoza jamii ya kiraia ya Kenya katika upinzani dhidi ya biashraa ya pembe za ndovu na yameandaa maelezo muhimu kuhusu suala hilo. Harvey Coroze, anayeblogu kwenye blogu ya Mfuko wa Amboseli kwa Tembo anasema:
Asasi ya ATE inapinga biashara hiyo. Tumekuwa tukifanya kazi na AZISE pamoja na watu wenye msimamo uanaoshabihiana chini ya mwamvuli wa Jukwaa la Tembo Kenya (KEF) kutoa taarifa za kimkakati kwa vyombo vya nchi za Afrika zenye tembo vinavyoitwa Umoja wa Tembo Afrika (AEC).
Katika makala hii ya blogu yake, Harvey ameweka viungo vya maelezo muhimu kuhusu suala hilo ya KEF ambayo unaweza kutaka kuyasoma ili kuona tatizo la pembe za ndovu na maana ya mapendekezo ya Tanzania/Zambia.