Namna Hali ya Hewa ya El Niño Inavyoathiri Maeneo ya Nyanda za Juu Nchini Myanmar

A child walks on the dried-up river bed of Thaminekham Dam near Aung Ban on April 28, 2016. Photo by Jpaing / The Irrawaddy

Mtoto akitembea pemebzoni mwa ukingo wa mto uliokauka wa bwawa la Thaminekham karibu na Aung Ban mnamo Aprili 28, 2016. Picha na Jpaing /Irrawaddy

Makala  hii ni ya The Irrawaddy, mtandado huru wa Habari wa nchini Myanmar, na inachapishwa tena Global Voices kama sehemu ya makubaliano ya kushirikiana maudhui.

Kwa kawaida, maeneo ya ukanda wa juu ya Shan huwa yanakuwa ya hewa nzuri kuliko maeneo makame ya ukanda wa kati na ya ukanda wa chini nchini Myanmar pamoja na kuwa, kwa mwaka huu, kama ilivyo tu kwa maeneo mengi ya nchi, kumekuwepo na hali mbaya ya hewa na ambayo haikutarajiwa ya El Niño.

Kwa upande wa Kusini mwa jimbo la Shan, chemichemi na maziwa yaliyokuwa yanatumiwa na wanajamii wazawa kwa ajili ya kuhifadhia maji ya mvua kwa matumizi ya nyumbani pamoja na shughuli za umwagiliaji, yamekauka tangu mwezi Februari, hali iliyowaacha wanavijiji wengi bila maji, hali inayosemekana kuwa mbaya zaidi kulinganisha na miaka iliyopita. Tun Kyi, mkuu wa Kijiji cha Kalaw Township’s Le Gaung, anaelezea hali ya mambo katika maeneo yake:

Ziwa lililopo karibu na kijiji chetu lilikauka miezi miwili iliyopita. Mwaka uliopita tuliweza kutumia maji ya Ziwa hili hadi mwezi Machi.

Katika kukabiliana na tatizo la kukosekana kwa maji, taasisi binafsi za nchini Myanmar kama vile Asasi ya Brighter Future Myanmar ilianza kusambaza maji ya kunywa vijijini. Asasi hii ya kipekee katika jimbo la Shan inachimba visima kwenye maeneo yaliyo na mwamba mgumu, imekuwa ikishirikiana na serikali ya Mynamar tangu mwaka 2004 kwa kupokea mashine za kuchimbia maji katika maeneo tambarare ya uwanda wa juu yaliyo na asili ya madini ya chokaa. Asasi hii inasema kwamba, katika siku za hivi karibuni imetumia kiasi cha dola za marekani milioni 1.5 kwa ajili ya kununulia mitambo yao wenyewe mipya ya kuchimbia maji na kuwa, hadi sasa katika Jimbo la Shan wameshachimba visima 100.

Bwawa lililokauka katika mji mdogo wa Pindaya huko Kusini mwa Jimbo la Shan, Aprili, 28. Picha na Jpaing /Irrawaddy

Wanakijiji wa Lel Gaung huko Kusini mwa Jimbo la Shan wakichota maji kutoka katika tenki la muda waliloletewa kwa hisani ya asasi ya mradi wa maji wa Brighter Future Maynmar. Picha na Jpaing /Irrawaddy

Washirika wa asasi ya Brighter Future Myanmar wakigawa maji katika kijiji cha Naung Bote karibu na Taunggyi. Picha na Jpaing/ Irrawaddy

Mwanaume akiteka maji katika tanki la jumuia huko Aung Ban. Picha na Jpaing /Irrawaddy

Exit mobile version