Ni Sikukuu ya Kuzaliwa Kristo (Noeli) Mjini Betlehemu

Ni sikukuu ya kuzaliwa Kristo mjini Betlehemu, katika ukanda wa Magharibi, Palestina, mahali alipozaliwa Kristo. Ni namna ipi nzuri zaidi ya kusherehekea tukio hili kwa kuwashirikisha picha pamoja na mitazamo ya watumiaji wa intaneti kuhusiana na tukio hili linalosherehekewa na mabilioni ya watu duniani kote.

Mwanahabari wa Israeli Joseph Dana alikuwa Betlehemu kuangalia mwanga wa miti ya Krismasi na alipakia mtandaoni picha ifuatayo:

Mwanga wa mti wa Krismasi mjini Betlehemu. Picha iliwekwa na @ibnezra katika mtandao wa Twita

Lauren Bohn aweka picha ya mti wa Krismasi aliyopigwa kwa ukaribu zaidi wakati wa sherehe hizi:

Mwanga mzuri wa mti wa Krismasi mjini Betlehemu, maoni @LaurenBohn katika Twita, wakati akiweka mtandaoni picha hii

Na Maath Musleh aweka mtandaoni picha zinavyoonesha jinsi mitaa ya Bethlehemu ilivyoangazwa katika maandalizi ya sikuu ya kuzaliwa Kristo:

Mitaa ya Betlehemu inavyoangazwa kwa mwanga wa taa za Krismasi, anatwiti @MaathMusleh, ambaye aliweka picha hii katika mtandao wa Twita

Ahmed Aggour, mchana wa leo aliweka picha hii ya mti:

Mti mzuri wa Krismasi kuliko mwingine wowote ule unaopatikana mjini Betlehemu. Heri ya sikukuu ya kuzaliwa Kristo. #Betlehemu #Palestina, alitwiti @Psypherize

Naye Daniel Aqleh aliweka mtandaoni video hii katika mtandao wa YouTube kuhusiana na sherehe ya kuwasha mti wa Krismasi iliyoambatana na kulipuliwa kwa fataki:

Heri ya Sikukuu ya Noeli kusherehekea Kuzaliwa kwa Kristo!

Exit mobile version