- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Serikali ya Cambodia Yasema Uchaguzi Ujao Utahusisha Watu Wengi na Utakuwa Huru na Haki—Lakini Asasi za Kiraia Zinasema Vinginevyo

Mada za Habari: Kambodia, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchaguzi, Uhuru wa Kujieleza, Utawala, Vyombo na Uandishi wa Habari
[1]

Picha ilipigwa kutoka video ya Youtube

Huria, walio wengi, kidemokrasia, uhuru, haki na amani.

Haya ni maneno yaliyotumiwa na ofisi ya habari inayofanya kazi pamoja na serikali ya Cambodia, ikieleza namna serikali itakavyoendesha uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika tarehe 29 mwezi Julai mwaka 2018 na kampeni zinaanza tarehe 7 Julai.
Video iliyotolewa [2]na kitengo cha habari na majibu ya haraka katika ofisi ya halmashauri ya mawaziri nayo ilijigamba kuwa uchaguzi ujao “utakuwa ni uchaguzi bora zaidi katika historia ya nchi.”

Inaonekana video ilikuwa inajaribu kujibu ukosoaji uliotolewa na makundi ya asasi za kiraia duniani juu ya kudidimia kwa hali ya demokrasia nchini. Chama cha watu wa Cambodia kimekuwa madarakani kwa miaka 33 chini ya uongozi wa waziri mkuu Hun Sen ambaye anafikiriwa amekuwa madarakani kwa muda mrefu kama mkuu wa nchi kutoka kusini mashariki mwa Asia.

Video inaonesha kwamba, uchaguzi utakuwa wa wazi kwa wagombea wote tofauti na maoni yaliyotolewa katika majukwaa ya kimataifa. Video ilijumuisha hotuba ya Hun Sen akielekeza maafisa kipindi cha kampeni kuvisaidia vyama vyote vilivyojiandikisha.

[1]

Waziri mkuu Hun Sen akihutubia. Picha ilipigwa kutoka kwenye video ya You Tube

Lakini kule neno la msingi ni “kuandikishwa.” Kwa kweli ni hakika kuwa vyama vilivyojiandikisha viko huru kushiriki katika chaguzi.

Lakini Novemba mwaka 2017, chama kikuu cha upinzani, Chama cha Ukombozi wa taifa Cambodia kilifutwa na mahakama kuu baada ya Hun Sen kukituhumu kuwa kimekula njama na nchi za nje kupindua serikali yake.

Viongozi wa juu wa chama cha ukombozi wa Taifa Cambodia aidha wamekimbia nchi au wamewekwa kizuizini kwa sasa na wabunge wake waliondolewa kwenye vyeo vyao na kufungiwa kutumia ofisi za umma kwa muda wa miaka mitano.
Video ineleza kuwa nchi ya Cambodia inatoa somo kwa nchi nyingine juu ya namna ya kuendeleza demokrasia ya walio wengi kwa kuonesha hali halisi ya mwaka 2013, [3] ambapo vilishiriki vyama nane katika uchaguzi mkuu. Serikali imesajili vyama vya siasa 20.

[1]

Cambodia ni mfano wa demkrasia ya walio wengi ? Picha iliyochukuliwa kutoka kwenye video ya You Tube

Pia, video inaonesha uwepo wa wangalizi wa kimataifa ambao watatembelea vituo vya kupigia kula bila kizuizi chochote. Serikali ilisema waangalizi 50,000 walialikwa [4] na waandishi wa habari 300 kutoka taasisi 35 wamethibitishwa kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka huu.

[1]

Video inadai kuwa tofauti na nchi nyingine, Cambodia na mahali ambapo waangalizi wa kimataifa hawatazuiwa. Picha iliyochukuliwa kwenye video ya YouTube. [/caption

Lakini video inashindwa kutaja kuwa mwezi Mei 2018, serikali imepitisha kanuni za maadili kwa waangalizi wa uchaguzi ambayo makundi ya vyombo vya habari yalisema ingezuia [5]waadishi wa habari kufanya kazi. Kanuni za maadili zinazuia waandishi wa habari kueleza “maoni binafsi au chuki” au kuendesha mahojiano yasiyo rasmi kwenye kituo cha kupigia kura.

Pia, kanuni za maadili zinatia hatia ya jinai chombo chochote cha habari kutangaza habari ambazo zinasababisha “vurugu na woga “katika uchaguzi.
Kama majibu kwa serikali, shilikisho la waandishi wa habari wa kimataifa walisema [6], “Kanuni hizi za maadili zimewaibia wananchi wa Cambodia nafasi ya habari muhimu za kujua maamuzi ya kisiasa kupata.”

Kipande kingine cha video kinaonesha uchaguzi unatangazwa kama tukio la amani “lisilokuwa na ugomvi wa maneno.”

[caption id="attachment_653446" align="aligncenter" width="792"] [1] Picha iliyochukuliwa kwenye video ya YouTube

Video haioneshi sheria baina ya wizara iliyopitishwa tarehe 28 Mei, 2018 ambayo imepanua uthibiti wa vyombo vya habari katika nchi. Sheria mpya hiyo inazipa mamlaka wakala wa serikali kufungia tovuti zenye madhui yanayofikiliwa kuwa “yakichokozi, yanayovunja mshikamano, yanayobagua na yenye nia yakuleta vurugu kudhoofisha usalama wa taifa, maslahi ya umma na amani ya jamii.”

Zaidi ya asasi za kiraia 116 zilizopo Cambodia zilisaini kauli ya [7] kukosoa sheria kwa hoja kwamba ” inatishia haki ya kutoingiliwa na uhuru wa kutoa maoni wa kila mtumiaji wa mitandao ya kijamii katika Cambodia na inaminya nafasi iliyoachwa kwa ajili ya mijadala ya umma kufuatia miezi ya mashambulizi ya uhuru wa vyombo vya habari.” Pia taarifa inasomeka:

Agizo linaweza kutumiwa kuzuia aina yoyote ya mjadala wa umma Cambodia. Kiukweli, wazo lolote ambalo mamlaka za serikali zinaona halikubaliki linaweza kuangushwa kwa kigezo cha “kuvunja mshikamano” au “kudidimiza amani ya jamii”.

Pamoja na kushambulia upinzani, pia serikali ya Hun Sen inashutumiwa kwa kuminya uhuru wa kujieleza baada ya kutoa agizo la kufunguliwa mashtaka ya kukwepa kodi [8] dhidi ya vituo vya redio na magazeti nchini ambavyo vimekuwa vikikosoa sana chama tawala.

Mashtaka hayo yalipelekea kufungiwa kwa magazeti mawili ya kujitegemea ambayo ni— Gazeti la kila siku la Cambodia na la Phnom Pehn Post. Baada ya kupata bili ya kodi kubwa mno, gazeti la Daily lilisimamisha [9] shughuli zake mwezi Septemba 2017, wakati mmilki wake alipoliuza [10] kwa kampuni ya Mahusiano ya umma ambayo inafanya kazi kwa niaba ya serikali.
Kwa uwazi, video inasistiza pia kuwa “mahudhurio ya wapiga kura sio kigezo cha kupima mchakato wa demokrasia.” Hata inaweka mifano ya mahudhurio hafifu ya wapiga kura katika nchi kama Marekani na Ufaransa. Inawezekana vitu hivi vimewekwa kutokana na ukweli kwamba chama cha Ukombozi wa taifa Cambodia kimewashauri wanachama na umma kususia chaguzi hizo.

Wakizungumza Umoja wa Mataifa mwishoni mwa mwezi Juni 2018, Tume ya kimataifa ya Majaji walieleza kwa ufupi [11] maoni ya makundi ya haki za binadamu juu ya kudidimia kwa demokrasia nchini Cambodia:

Mamlaka zinaendelea na uvunjaji wa mfumo wa haki kwa kunyamanzisha asasi za kiraia,vyombo vya habari vya kujitegemea, vyama vya upinzani, na hata watu binafsi.
Serikali imetishia kukamatwa kwa mtu yeyote ambaye anatoa wito wa kugomea uchaguzi uliokubaliwa na wananchi wote. Imefahamika kuwa kuna kundi la wafanyakazi wanaofuatilia na kudhibiti habari zote katika tovuti na mitandao ya kijamii. Watu wa kawaida wanakamatwa, kushtakiwa na kuwekwa kizuizini chini ya sheria mpya.

Hapa chini ni video nzima [1]iliyotolewa na kitengo cha habari na majibu ya haraka katika ofisi ya halmashauri ya mawaziri: