- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Wa-Belarusi Waamua Kuchapa Kazi Wakiwa Uchi (Kutii Wito wa Rais)

Mada za Habari: Ulaya Mashariki na Kati, Belarus, Harakati za Mtandaoni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Upiga Picha, Vichekesho, RuNet Echo
Belarusian Internet users stripped in their workplaces to respond to the President's call to put more effort into their work. Image from Instagram.

Watumiaji wa mtandao wa intaneti wa ki-Belarusi waliamua kuvua nguo zao wakiwa kazini kutii wito wa Rais wa kuongeza bidii kwa kazi zao. Picha kutoka mtandao wa Instagram.

Wananchi wa Belarusia hawana kawaida ya kutii amri za rais wao aliyedumu madarakani kwa kuda mrefu, Alyaksandr Lukashenka. Kwa hakika, utawala wake wa kiimla nchini humo unaokosolewa sana. Lakini inavyoonekana, kila sheria ina mazingira fulani ya kukiukwa.

Mnamo Juni 22, Lukashenka alizungumza kwenye mkutano unaofahamika kama ‘Wa-Belarusi Wote’, na alimalizia hotuba yake kwa kuwataka wananchi wote kujibidiisha katika kujitafutia maisha bora.

Наша жизнь в простом. Надо раздеваться и работать. До седьмого пота. Не будет этого – погибнем.

Maisha yetu yanahusu mambo rahisi na ya kawaida. Lazima tuvue nguo tuchape kazi. Tuchape kazi hata jasho litutoke. Tusipofanya hivyo, ndugu zangu tutapotea.

Video [1] ya hotuba ya Lukashenka imesambaa sana kwenye mitandao ya kijamii, huku watumiaji wa mitandao hiyo wasioamini kama kwenye Rais aliyatamka maneno hayo na kujaribu kuthibitisha kama kweli Rais alitumia neno “kuvua nguo” (раздеваться) na sio neno jingine lenye matamshi kama hayo lenye maana ya “ku[ji]endeleza” (развиваться).

Lakinihotuba iliyoandikwa [2] na kuwekwa kwenye tovuti ya ikulu ya nchi hiyo inathibitisha kwamba kweli Rais alimaanisha wananchi wavue nguo. Kwa hiyo wananchi wakaamua kweli kutekeleza agizo hilo.

Punde, mitandao ya kijamii ikafurika [3] picha na video (nyingi zikiwa za vijana) wa ki-Belarusi wakiwa maofisini na makazini, uchi, huku wakifunika kidogo sehemu zao za siri kwa meza, kompyuta mpakato, na vifaa vingine na kuonekana wakiendelea na kazi zao. Tovuti ya habari nchini humo iitwayo CityDog ilikusanya [3] baadhi ya picha hizo kwenye mitandao ya kijamii.

#раздеватьсяиработать #ялюблюсвоюработу #чутьчтомыодеты #четкаяконспирация #minsk [4]

A photo posted by Маргарита Воропаева (@margo_voropaeva) on

Батька сказал раздеться и работать, мы разделись и работаем)
#раздеватьсяиработать
#корпоративныйстиль
#irmcreative

A photo posted by @ssnnooppooyy on

Batka (jina la utani la Lukashenko) alisema tuvue nguo tufanye kazi, kwa hiyo tumeamua kubaki uchi tuchape kazi.

#раздеватьсяиработать и мы последуем совету!)) #Fistashki #коллегидрузья [5]

A photo posted by @budenis on

Tunazingatia ushauri wa Rais))

Все только для того, чтобы поднять экономику страны. #раздеватьсяиработать #lukashenko #belby #belbeznalby #computer #shop #work #ignat #жилистый #флешмоб [6]

A photo posted by Alexandr Ignatovich (@fun_bayern) on

Tunafanya lolote liwezekanalo kukuza uchumi wa nchi.

Maelfu ya wa-Belarusi wameweka picha kwenye mitandao ya Instagram [7], Facebook [8], na Twitter [9] kwa kutumia alama ishara ya #раздеватьсяиработать (#vuanguofanyakazi).

#раздеватьсяиработать #музейбровки #ниднябезбровки #музей [10]

A photo posted by Музей Петруся Броўкі (@museum_brovka) on

Сегодня я прополола клубникуА как ты исполнил государственное поручение #раздеватьсяиработать? Не коси, #раздевайсяиработай [11]

A photo posted by Viktoriya Akvinskaya (@akvinskaya) on

Nilichuma matunda leo. Nikajiuliza nawezaje kutekeleza amri ya Rais?

Vituko vya picha hizo vilishika kasi kiasi cha kuwavutia watumiaji wa mtandao katika nchi nyingine Urusi kushiriki [12].

Поддерживаю флешмоб сябров #раздеватьсяиработать ! Ибо пятница! #живебеларусь #лукашенко #пятница #работа [13]

A photo posted by Hanna Hrabarska (@anya_grabarskaya) on

Tunaunga mkono harakati za wa-Belarusi!

Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa intaneti walikwenda hatua kadhaa mbele na kuweka video [14] za nyimbo [15] zilizotungwa mahususi kwa wakati huo. Kwenye video hizo, wananchi wanaimba wakiwa karibia na uchi. Hatua hiyo inaonekana kutuma ujumbe kwamba viongozi wa nchi wnaahitaji kuwa makini na kile wanachokitamka hadharani.