- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Naijeria: Kampeni ya #Bringourgirlsback

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Naijeria, Dini, Habari za Hivi Punde, Harakati za Mtandaoni, Maandamano, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Upiga Picha, Utawala, Vijana, Wanawake na Jinsia

 


Bango la kampeni. Wasichana 234 wenye umri kati ya miaka 16-18 walitekwa nyara takribani wiki mbili zilizopita nchini Naijeria: #bringourgirlsback. Chanzo: Ukurasa wa Facebook #bringourgirlsback ‬- Kwa Matumizi ya Umma

Katikati ya mwezi Aprili, zaidi ya wasichana 200 wa shule walitekwa nyara [1]kutoka shule ya sekondari iliyoko eneo la Chibok, Naijeria, kitendo kinachodaiwa kufanywa na Boko Haram, kundi la kigaidi lililoko katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo. Ingawa baadhi ya wasichana 57 wameweza kutoroka, bado wengine wengi wako mikononi mwa watekaji nyara. Tarehe Aprili 30, wanawake Wanaijeria waliandaa maandamano katika miji kote nchini Naijeria kushurutisha serikali iongeze jitihada zake za kuwaokoa wasichana hao. Tovuti ya Waandishi wa Habari ya Sahara ilichapisha picha [2] kutoka Kaduna, Nigeria. Wanablogu Wanaijeria pia walifungua ukurasa wa mtandao wa Facebook wakitumia alama ashiria #bringourgirlsback [3] kutoa wito wa kueneza hasira kwenye mtandao dhidi ya hatua hii ya jinai ya waasi wenye msimamo mkali.