- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Gharama na Faida ya Kombe la Dunia Nchini Brazil

Mada za Habari: Amerika Kusini, Brazil, Colombia, Michezo, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchumi na Biashara

Blogu [1] ya Daniel Bustos kutoka Colombia kuhusu uchumi wa Kombe la Dunia nchini Brazil na baada ya kugusia suala lisilo epukika la rushwa, inasema:

Hatimaye, Brazil itatumika kama “panya” kwa mataifa ya Amerika ya Kusini ambayo yalikuwa na ndoto kuwa siku moja itaandaa tukio hili kubwa, itatumika kuuliza kama Brazil itapata mapato mazuri na miundombinu yote iliyobadilishwa au kama, kinyume chake, lilikuwa ni kosa kubwa na la gharama kubwa, kama itafanya nchi kama yetu kutafakari juu ya kile kinachofanywa katika serikali katika masuala ya miundombinu, ajira, elimu, na bila shaka, kuwekeza katika michezo ili siku moja Kombe la Dunia litaweza kuandaliwa.

Posti iliyoainishwa ilishiriki katika #GVBlogsMonday [2]ya pili [es] Mei 12, 2014.