- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Vyombo Vikuu vya Habari Vyaihujumu Facebook

Mada za Habari: Asia ya Kusini, Sri Lanka, Maandamano, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vyombo na Uandishi wa Habari

Mwanablogu wa Teknolojia Amitha Amarasinghe [1] anadai kwamba mtandao wa Facebook unapewa taswira hasi na vyombo vikuu vya habari nchini Sri Lanka kwa vichwa vya habari kama “Mwanafunzi ajiua shauri ya picha iliyowekwa Facebook”, “Mapenzi ya Facebook yaishia na kifo” na kadhalika.

Ghafla tu, kuna mwongezeko mkubwa wa maudhui yanayotoa taswira hasi ya mtandao wa Facebook na Mitandao mingine ya kijamii. Kama ukichunguza habari hizi, [utagundua kuwa] vyombo vya habari vya hapa vinaitumia “Facebook” kama sehemu ya “habari”, lakini vikishindwa kuoanisha sababu za kijamii, kitamaduni, na kisiasa zinazosababisha matukio hayo.