Ili kuondoa uhaba wa hosteli kwa ajili ya wanafunzi unaovikabili vyuo vikuu barani Ulaya, baadhi ya vyuo vikuu nchini Denmaki [2], Ujerumani, Ufaransa [3] (Le Havre) [fr] na Uhispania vimejaribu kubadili makontena na kuyafanya yawe hosteli za wanafunzi [4]. Makontena yanaonekana kufaa kwa sababu hayana gharama kubwa na yanazoeleka kirahisi. Hata hivyo, taasisi kadhaa tayari zimeibua masuala kadhaa [5] [fr] kuhusiana na mifumo ya kuyapasha “makazi” hayo joto pamoja na masuala ya usalama.
UBUNIFU: Makontena Yatumika Kama Hosteli za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Ulaya
· Imeandikwa na Lova Rakotomalala Imetafsiriwa na Mghosya
Mada za Habari: Ulaya Magharibi, Denmaki, Ufaransa, Uhispania, Ujerumani, Elimu, Mawazo, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vijana