- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Hali ya Uhuru wa Dini Nchini Maldivi

Mada za Habari: Asia ya Kusini, Maldives, Dini, Elimu, Maendeleo, Sheria, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala

Maldivi ni miongoni mwa nchi za kwanza kwenye orodha ya serikali zinazozuia uhuru wa dini [1]. Ni lazima raia Wamaldivi wawe Waislamu, na hawawezi kufuata dini yoyote isipokuwa Uislamu. Wageni wasio Waislamu [2] hawawezi kupiga kura, kuabudu hadharani, kupata uraia, wala kutumikia umma.

Kwa maoni ya Mwanahabari Hilath Rasheed [3], huenda nchi ya Maldivi ikashindwa kuegamisha uhuru wa dini katika miaka 50 ijayo, hadi kubadilika kwa mawazo ya vizazi vipya vya Wamaldivi.