23 Disemba 2013

Habari kutoka 23 Disemba 2013

China: Mashindano ya “Akina Mama Wanaotamanisha”

  23 Disemba 2013

Sina Weibo, tovuti ya Kichina inayofanana na Twitta, imeandaa mashindano ya “Akina Mama Wanaotamanisha.” Picha za washindani zinaonyesha wazi kwamba wengi wao sio akina mama halisi. Hata hivyo, hizo picha zinatuambia mengi kuhusu uhusiano wa kijinsia nchini China. Soma mengine kwenye tovuti ya Offbeat China.

Changamoto za Huduma ya Afya kwa Familia Katika Apatou, French Guiana

  23 Disemba 2013

Henri Dumoulin, mchangiaji wa Global Voices, anakumbuka kukaa kwake huko Apatou, French Guiana,sehemu iliyoko katika msitu wa Amazon. Anaelezea jinsi gani, kama daktari wa mpango wa ulinzi wa Afya ya Mama na Mtoto huko, alivyokuwa akitegemea ushirikiano rasmi na mfumo wa afya wa Suriname na kutizamwa mazingira ya lugha mbalimbali...

Hali ya Uhuru wa Dini Nchini Maldivi

  23 Disemba 2013

Maldivi ni miongoni mwa nchi za kwanza kwenye orodha ya serikali zinazozuia uhuru wa dini. Ni lazima raia Wamaldivi wawe Waislamu, na hawawezi kufuata dini yoyote isipokuwa Uislamu. Wageni wasio Waislamu hawawezi kupiga kura, kuabudu hadharani, kupata uraia, wala kutumikia umma. Kwa maoni ya Mwanahabari Hilath Rasheed, huenda nchi ya...