- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

China: Miitikio ya Raia wa Mtandaoni Kufuatia Muswada wa Sheria ya Kurithi Kodi

Mada za Habari: Asia Mashariki, China, Sheria, Uandishi wa Habari za Kiraia

Watumiaji wa mtandao nchini China walionyesha kutokuridhishwa kwao na muswada wa sheria unaopendekeza uwezekano wa kurithiwa kodi zinazoanzia yuan RMB 800,000 [yuan ni sarafu ya nchi hiyo]. Badala ya kuziba pengo la kipato miongoni mwa wananchi, watumiaji wa mtandao wanaamini kuwa sheria mpya inakusudia kuiba fedha kutoka kada ya wafanyakzi. Zaidi [1] kutoka kwenye mtandao wa Offbeat China.