- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Lebanon: Mwanablogu Apata Kipigo kwa Kupiga Picha

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Lebanon, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza

Mwanablogu wa ki-Lebanoni Habib Battah anaeleza namna alivyoshikiliwa bila hiari, akilazimishwa kufuta picha katika kamera ya simu yake na kudhalilishwa mfululizo katika posti hii [1] inayohusiana na ripoti ya Beirut. Aliporipoti suala hilo katika kituo cha polisi mahali alipokuwa, mafisa wanaohusika walimkana na kumgeuzia kibao yeye. Anaongeza:

Walikuwa sahihi. Kama watu walikuwa eneo la tukio walikuwa tayari kunipa kichapo ili kumridhisha bosi wao, watu hao lazima wangeweza kudanganya kumridhisha. Na nilivyopigwa, hakuna mtu mtaani angekuwa tayari kutoa ushahidi namna walivyoninyanyasa namna ile.

Niliondoka polisi nikijisikia kuwa raia wa ki-Lebanoni hawalindwi na sheria. Matajiri wanaweza kutukanyaga kama sisimizi, kama tutajaribu kuwakasirisha.