- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Watu 60 Wauawa kwa Msongamano nchini Abidjan

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Cote d'Ivoire, Habari za Hivi Punde, Harakati za Mtandaoni, Majanga, Mwitikio wa Kihisani, Uandishi wa Habari za Kiraia

Magogo ya miti yaliyokuwa yameanguka barabarani yanaonekana kusababisha msongamano mkubwa na ulioua watu 60 na kujeruhi wengine 49 wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya mjini Abidjan, Côte d'Ivoire. Kutokana na ukweli kuwa eneo hilo halikuwa na mwanga wa kutosha inawezekana ndio sababu iliyochangia tukio hilo la msongamano ulisababisha mkanyagano wa watu.

Israel Yoroba jijini Abidjan anaripoti kuhusu msongamano huo wa kutisha [1] [fr] wakati watu wengi wakiwa wamekusanyika kusubiri kushuhudia milipuko ya fataki kuashirika mwaka mpya katika wilaya ya Plateau. Alama habari #drameplateau [2] ilianzishwa kutoa nafasi ya kupatikana kwa habari za wakati huo huo kuhusu tukio hilo la kusikitisha na namna ya kuwasaidia waathirika. Hili nijanga la tatu la namna hii tangu mwaka 2009 [3] [fr] nchini Côte d'Ivoire.