2 Januari 2013

Habari kutoka 2 Januari 2013

Bangladeshi: Msichana Mwingine Mzawa Abakwa na Kisha Kuuliwa.

  2 Januari 2013

Kwa mara nyingine msichana mzawa ameuawa nchini Bangladesh baada ya kubakwa kikatili. Mhanga huyo, Khomaching Marma (14) alikuwa mwanafunzi wa darasa la nane. Ubakaji huu wa kikatili uliosababisha mauaji kwa mara nyingine tena umeamsha hasira na ghadhabu nchini kote. Watumiaji wa mtandao pia wanapinga vikali vitendo hivyo.

Watu 60 Wauawa kwa Msongamano nchini Abidjan

Magogo ya miti yaliyokuwa yameanguka barabarani yanaonekana kusababisha msongamano mkubwa na ulioua watu 60 na kujeruhi wengine 49 wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya mjini Abidjan, Côte d'Ivoire. Kutokana na ukweli kuwa eneo hilo halikuwa na mwanga wa kutosha inawezekana ndio sababu iliyochangia tukio hilo la msongamano ulisababisha mkanyagano...

Kusherehekea Mwaka 2012 na Sauti za Dunia

Kadiri mwaka 2012 unavyofikia tamati, tungependa kutoa shukrani zetu kwa kazi nzuri, ubunifu pamoja na kuonesha kujali mambo mengi katika jumuia ya Sauti za Dunia. Mwaka 2012 umekuwa ni mwaka wa ukuaji wa kasi kabisa na wa mafanikio kwa Sauti za Dunia ( Global Voices). Yafuatayo ni baadhi tu ya mafanikio: