- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Msumbiji: Je, Zana za Uandishi wa Kiraia Zimeua Blogu?

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Msumbiji, Uandishi wa Habari za Kiraia

Katika mfululizo mfupi [1] wa makala zake, Profesa Carlos Serra anabainisha baadhi ya sababu zinazoeleza kwa nini blogu za Msumbiji zinaendelea kupungua siku hadi siku. Msomaji mmoja anatoa maoni [2] akidhani kwamba kublogu kunahitaji kazi kubwa katika kuhakikisha kuwa habari mpya zinaendelea kuwepo sambamba na kiwango cha habari hizo. Wakati Serra anasema kwamba zana za uandishi wa kiraia (kama vile twita na facebook) zinaweza kulaumiwa kusababisha hali hii [3], pamoja na faida za matumizi ya zana hizo [4].