12 Julai 2012

Habari kutoka 12 Julai 2012

Wananchi wa Mexico Wanamchagua Rais Mpya

Mnamo tarehe 1 Julai, Wa-Mexico walipiga kura kumchagua rais wao mpya. Punde tu kura zilipoanza kupigwa, watumiaji wa mtandao wa intaneti walianza kutoa mawazo na uzoefu wao. Walipanga pia namna tovuti na alama ishara za mtandao wa twita zitakavyotumika kukusanya taarifa juu ya udanganyifu na nyendo zilizo kinyume cha sheria wakati wa uchaguzi huo.

12 Julai 2012

Palestina: Makala Kuhusu Kifo cha Arafat yaibua maswali

Kituo cha habari cha Al Jazeera hivi karibuni kilionyesha makala iliyohusu kifo cha utata cha rais wa Palestina Yasser Arafat kilichotokea mjini Paris mnamo Novemba, 2004. Makala hayo yanadai kwamba kiongozi huyo hakufa kifo cha kawaida, ila aliwekewa sumu ya poloni, madai ambayo yanaibua maswali mengi.

12 Julai 2012