- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Lebanoni: Utawala wa Dinosauri

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Lebanon, Haki za Binadamu, Harakati za Mtandaoni, Siasa, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia, Ubaguzi wa Rangi, Uhuru wa Kujieleza

Punde baada ya matukio ya [1] unyanyasaji [2] ya hivi karibuni nchini Lebanon, Msemo wa “Utawala wa Dinosaurs” ulianza kutumika na wanaharakati wa mtandaoni kwenye kampeni dhidi ya uvamizi wa namna hii katika mitandao yao. Mwanablogu wa Lebanon Tonyanaeleza maana ya msemo huo katika makala yenye jina”“Jinsi ya Kummudu Dinosauri [3]“:

“الديناصورات” هو اللقب الذي أطلقه بعض الناشطين اللبنانيين مؤخراً على أقطاب السياسة والأجهزة الأمنية في لبنان بعدما تركوا كل مشاكل البلاد وتفرّغوا لقمع الحريات وكمّ الأفواه واقتحام المسرحيات ومنع الكتب والأفلام السينمائية واعتقال الناشطين وممارسة العنصرية ضد الأجانب. اللقب هو على سبيل المزاح طبعاً، لكن إصرارنا على إسقاطهم لا يدخل أبداً ضمن إطار المزاح، بل هو ضمن إطار التراجيديا التي لا مفرّ لهم منها. “الديناصورات على أشكالها تقع” هو عنوان معركتنا
“Dinosauri” ni jina wanalopewa wanasiasa na wanaharakati wa mtandaoni siku hizi. Hii imetokea kutokana na wao kuacha kushughulikia matatizo ya msingi ya nchi na kushindia kunyima uhuru watu kwa; kunyamazisha watu, kupiga marufuku vitabu, tamthilia na filamu, kukamata wanaharakati na kufanya ubaguzi wa rangi hasa kwa wageni. Jina ni la utani tu, lakini malengo yetu ya kuwaangamiza si utani hata kidogo, na hayazuiliki. “Dinosauri wafananao huruka pamoja” ni jina la vita hivyo.