Habari kuhusu Ufaransa

Martinique: Uhuru na “Ubeberu” wa Kifaransa

  26 Februari 2009

Wakati harakati za wafanyakazi zinaendelea huko Martinique na Guadeloupe, wanablogu wa Martinique wanapima uhuru wa Idara za Ng'ambo utamaanisha nini. Le blog de [moi] anaona dhana ya kuwa Martinique haiwezi kujitegemea ni dhana inayotusi na ya kibeberu. Wasomaji wake wanadhani kuwa ukweli wa kisiwa chochote kidogo ni kuwa kila siku kitakuwa katika kivuli cha wengine.

Madagascar: Kuishi ughaibuni hubadili uhusiano

Katika makala iliyochapishwa mwezi Machi, wachumi William Easterly na Yaw Nyarko wanaeleza kwamba katika nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara, kiasi cha fedha kinachotumwa na wahamiaji wanaotoka bara hilo ni wastani wa asilimia 81 ya misaada ya fedha kutoka nchi za kigeni kwa kila nchi. Dhima ya waMadagascar walio...

Macho ya Kimataifa kwenye Uchaguzi wa Marekani

Kadiri uchaguzi wa Marekani unavyokaribia, ndivyo kadiri macho ya kimataifa yanavyozidi kuelekezwa katika sera za nje za taifa hilo na wagombea wake wakuu. Kazimiradi kama vile ile ya Collective Journalism inayofanywa na Current TV (Uandishi wa Habari wa Umma wa Current TV) na Global Voices' Voices Without Votes (Mradi wa Global Voices - Sauti Zisizo na Kura) zimechukua jukumu la kukusanya taarifa na kuzipa mtazamo wa kimataifa katika masuala ya ndani ya sehemu fulani tu ulimwenguni.