Habari kuhusu Ulaya Magharibi kutoka Novemba, 2009
Afya Duniani: Siku ya Vyoo Duniani Yatoa Harufu
Ingawa inaweza kusikika kama masihara, Siku ya Vyoo Duniani inatilia maanani kwenye suala ambalo si la mzaha linalowakwaza karibu nusu ya watu wote duniani – ukosefu wa vyoo na mfumo wa usafi.
Ufaransa: Tuzo ya Fasihi Yaja na Masharti
Mwanzo wa msimu wa Fasihi ya Kifaransa mwaka huu ulishuhudia mwandishi wa riwaya na michezo ya kuigiza mwenye asili ya Kisenegali na Kifaransa Marie N’Diaye akipewa tuzo iliyosuburiwa sana ya Prix Goncourt. Lakini, N’Diaye na familia yake walikwishahamia mjini Berlin miaka miwili iliyopita, hasa kutokana na siasa za rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy. Mwaka jana, jopo la tuzo hii yenye hadhi walizusha hisia kali pale walipomchagua mwandishi wa Kiafghani Atim Rahimi, kwa kitabu chake cha Kifaransa, Syngué Sabour. Je hii itakuwa ni fursa nyingine ya kusherehekea mchanganyiko wa aina mbalimbali katika jamii inayobadilika ya Kifaransa? Au itakuwa ni wasaa utakaoharibiwa na utete wa tukio?
Karibea: Tuzo za Fasihi ya Kifaransa
Wiki hii, waandishi wawili wenye asili ya Kiafrika wanaoandika kwa Kifaransa walipewa tuzo mbili zenye kuheshimika sana katika fasihi ya Kifaransa: Ulimwengu wa blogu za wanaozungumza Kifaransa katika Karibea umekuwa...
Finland: Suala la Lugha
Nordic Voices anaandika kuhusu ‘suala la lugha” huko Finland.
Misri: Haki ya Kijerumani kwa Marwa El Sherbini
Muuaji wa Marwa El-Sherbini, mwanamke wa Kimisri ambaye alichomwa visu mpaka kufa na muhamiaji mwenye asili ya Urusi na Ujerumani, Alex Wiens, ndani ya mahakama huko Ujerumani, amehukumiwa kifungo cha maisha, bila uwezekano wa kuachiwa mapema. Haki hatimaye imetolewa na muuaji anaadhibiwa, wanasema wanablogu wa Misri.
Video: Dunia Yaadhimisha Kuanguka kwa Ukuta wa Berlini
Leo ni Kumbukumbu ya 20 ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlini, kizingiti madhubuti cha kiusalama ambacho kiliwahi kuligawa jiji la Berlini katika pande mbili za Mashariki na Magharibi huko Ujerumani. Leo tunaonyesha baadhi ya picha za video zinazotoka pande mbalimbali za dunia zinazopandishwa ili kusherehekea siku hii na nini ukuta huo ulimaanisha siyo Ujerumani tu bali duniani kote.
Ujauzito na Magereza: Afya na Haki za Wanawake Magerezani
Mapambano bado yanaendelea kuhakikisha haki za binadamu kwa wanawake wajawazito duniani pote, ni inaelekea kwamba katika mchakato huo, wanawake waliopo magerezani wanasahauliwa. Je ni hatua zipi zilizochukuliwa kuhakikisha kuwa nao wanaangaliwa kwa utu, kwa kuzingatia uhai wanaoubeba.