Habari kuhusu Ulaya Magharibi kutoka Januari, 2009
Ugiriki: Malalamiko Kuhusu Usafirishwaji wa Silaha kuelekea Israeli
Wakati vita vikiendelea huko Gaza, taarifa zilizotolewa mwanzoni mwa mwezi kuhusu shehena kubwa ya silaha kutoka Marekani kuelekea Israeli kupitia bandari ya Astakos huko Ugiriki zimezua kelele kutoka kwa wanablogu wa Kigiriki. Wanablogu hao walitumia huduma ya Twita kuchunguza swala hilo na kuitia shinikizo serikali ya Ugiriki kusimamisha usafirishwaji wa silaha hizo.
Palestina: Shule ya Umoja wa Mataifa Yashambuliwa na Makombora ya Israeli, Zaidi ya 40 wafariki
Takriban majira ya saa 12 za jioni (GMT +2), Idhaa ya Kiingereza ya Al Jazeera iliripoti kuwa shule moja ya Umoja wa Mataifa ilipigwa wakati makombora mawili ya vifaru yalipolipuka nje ya shule hiyo. Shule hiyo, iliyopo Jabaliya, ilianza kutumiwa kama makazi ya raia wa Gaza waliozikimbia nyumba zao au waliopoteza makazi yao. Zaidi ya watu 40 wameuawa. Jillian York anawasilisha maoni ya mwanzo kabisa katika ulimwengu wa blogu na twita.