Habari kuhusu Zimbabwe kutoka Disemba, 2011

Zimbambwe: Hasira wakati Mzee Mugabe Anapowania Uchaguzi wa 2012

  15 Disemba 2011

Chama cha ZANU –PF (Zimbabwe African National Union - Patriotic Front) kimempitisha Robert Mugabe kuwa mgombea wake kwa ajili ya uchaguzi wa rais unaotazamiwa kufanyika mwaka ujao. Kama uchaguzi utafanyika mwakani, Mugabe atakuwa na umri wa miaka 88 na atakuwa Mwafrika wa pili mzee zaidi kugombea katika uchaguzi wa rais. Kupitia Twita na Facebook wa-Zimbabwe wameonyesha hasira na kutokuamini kilichotokea.