Habari kuhusu Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara
Mnigeria Abubakar Idris Dadiyata Bado Hajapatikana, Ni Mwaka Mmoja Sasa Baada Ya Kutekwa
“Jinsi gani Dadiyata anaweza kupote kwa mwaka mzima ndani ya Nigeria na serikali haina wasiwasi na jambo hili, zaidi inatafuta kujiosha badala ya kuwajibika kumtafuta?”
Wanafunzi na Mwalimu Wao Watekwa Huko Kaduna Naijeria, Wakati Maharamia Wenye Silaha Wakifanya Vurugu na Mauaji
Maharamia wenye silaha waliowateka wanafunzi wanne na mwalimu wao kutoka Damba-Kasaya, jimbo la Kaduna nchini Nigeria wanadai fedha ili waweze kuwaachilia huru mateka hao
Makubaliano Ya Amani Ya Kihistoria Nchini Sudani Yafanyika Kukiwa na Mafuriko Ya Kihistoria
Makubaliano ya amani ya Kihistoria ya vikundi vya waasi Sudani yamefanyika kukiwa na mafuriko ya Kihistoria yaliyosababisha majanga. Nini hasa mkakati wa serikali kuyarahisisha maisha?
Waandishi Wa Habari wa Msumbiji Waachiwa Huru Baada ya Kukaa Kizuizini Kwa Miezi Kadhaa Bila Kufunguliwa Mashtaka
Amade Abubacar na Germano Adriano walikuwa kizuizini tangu Januari lakini walishtakiwa tu hapo Aprili 16. Kwa sasa wanasubiri shauri lao lisikilizwe wakiwa chini ya uangalizi.
Waandishi wa habari wanawake nchini Uganda wanabeba ‘mzigo maradufu’ kutokana na mashambulizi ya mtandaoni pamoja na udhalilishaji
Waandishi wa habari wanawake nchini Uganda wanaubeba mzigo maradufu wa dhuluma inayotokana na jinsia mtandaoni ikiwa ni pamoja na vitisho vinavyohusiana na kuripoti taarifa za kisiasa. Vitisho hivi vinavyoendelea vimesababisha waandishi wa habari wanawake kujiondoa kwenye nyuga za umma.
Kukifanya Kiswahili kionekane: Utambulisho, lugha na Mtandao
Kiswahili ni lugha ya Kiafrika inayozungumzwa sana, lakini muonekano wake mtandaoni ni finyu zaidi. Mwanaharakati wa lugha kutoka Kenya Bonface Witaba anapambana kubadili hali hii.
#MatrikiUtambulisho: Mazungumzo ya Twita yanayoangazia utambulisho na haki za kidijitali barani Africa
Wanaharakati kutoka Burkina Faso, Nijeria, Afrika Kusini na Kenya, wataongoza mazungumzo kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia lugha zao za asili kuhusu masuala ya lugha, makabila na haki za kidijitali barani Afrika.
Serikali ya Zimbabwe yaendelea kutumia habari za mtandaoni kama silaha ya kukandamiza haki za raia
Serikali mpya, iliyoongozwa na Emmerson Dambudzo Mnangagwa,iling’amua mara nguvu ya mitandao ya kijamii. Kama waziri wa zamani wa usalama wa nchi, Mnangagwa pia alitambua umuhimu na nafasi ya upotoshaji taarifa katika nyanja za kisiasa za Zimbabwe.
Je, Uganda itazima intaneti kadiri upinzani unavyozidi kuwasha moto kuelekea uchaguzi mkuu wa 2021?
Wakati uchaguzi wa 2021 unapokaribia, kuna uwezekano mkubwa kuwa utawala wa Uganda utaendeleza ukandamizaji wa wapinzani, ikiwa ni pamoja na kufunga mitandao ya kijamii.
Shule pekee ya muziki Zanzibar hatarini kufungwa
Kwa zaidi ya wanafunzi 1,800 waliowahi kupitia mafunzo ya shule ya DCMA, hii ndiyo shule pekee ya muziki wanayoifahamu, ambako wanaweza kujifunza na kukua kama wasanii na wanamuziki mahiri.