· Disemba, 2009

Habari kuhusu Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kutoka Disemba, 2009

Ghana: Rais Atta Mills Dhidi ya Chama Chake Mwenyewe?

  13 Disemba 2009

Katika miezi michache kuelekea uchaguzi wa Rais Hohn Evans Atta Mills, wa-Ghana wengi, pamoja na wale walio nje ya nchi, waliohofu kwamba ushindi wa chama cha New Democratic Congress (NDC) ungeweza kugeuka kuwa utawala mwingine wa mwanzilishi wa chama hicho na mtawala wa zamani wa kijeshi, Rais Jerry John Rawlings.

Ghana: Fikra Juu ya Mkosi Unaoyanyemelea Mafuta

  13 Disemba 2009

Fikra Juu ya Mkosi Unaoyanyemelea Mafuta: “kwa dibaji, Ninasema kuwa ninaamini katika haki za mali (ardhi na majengo), serikali yenye mipaka pamoja na mipango huru, japokuwa ni lazima niseme kuwa si rahisi kuidhibiti mikataba ya mafuta, hasa pale haki za mali (ardhi na majengo) zinapohusika.”

Guinea: Jaribio la Kumuua Kiongozi wa Kijeshi Dadis Camara

  6 Disemba 2009

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari, Kapteni Dadis Camara, kiongozi wa kikundi cha jeshi kilitwaa madaraka nchini Guinea mwezi Disemba 2008, alipigwa risasi na kujeruhiwa na mmoja wa wasaidizi wake jana mjini Conakry. Wasomaji wengi wa RFI wanaodai kuwa Camara anawajibika kwa mauaji ya waandamanaji wa upinzani yaliyotokea tarehe 28 Septemba, wanaoana kuwa haki imetendeka.

Mwanamuziki mmoja wa Afrika Mashariki awashinda wengine wote kwa umaarufu wa mtandaoni duniani

  5 Disemba 2009

Si wengi wanamfahamu kama Mwanaisha Abdalla bali Nyota Ndogo, ni jina linalojulikana kwenye kila nyumba katika Afrika Mashariki. Amekuwa akikusanya mashabiki wa mtindo wake wa kipekee wa Afrika Mashariki kwa miaka zaidi ya 4 sasa. Blogu yake, katika upande mwingine, imekuwa ikiendeshwa kwa muda wa miaka 3. Hapana shaka kuwa blogu hiyo imechangia ongezeko la kambi ya mashabiki kwenye mtandao wa intaneti.

Ghana: Nani atanufaika na mafuta?

  5 Disemba 2009

Wakati Kampuni ya mafuta ya Uingereza Tullow Oil ilipotangaza uvumbuzi wake wa kiasi cha mapipa milioni 600 ya mafuta nchini Ghana mwaka 2007, ulimwengu wa wanablogu uliitikia kwa maoni yanayotofautina kati ya matumaini na hali ya hofu hasi.