· Novemba, 2009

Habari kuhusu Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kutoka Novemba, 2009

Angola: Gharama za Juu za Maisha Mjini Luanda

  10 Novemba 2009

Gharama kubwa ya maisha nchini haieleweki: viashiria vya maendeleo vya hali ya juu havishabihiani na hali ya kifedha ya Waangola wengi na havitafsiriki katika viwango vya maisha vya wasio na hali nzuri kiuchumi.

Naijeria: Ken Saro-Wiwa Akumbukwa

  10 Novemba 2009

Chidi Opara anamkumbuka Ken Saro-Wiwa, Mwandishi wa Kinaijeria, mwanaharakati wa mazingira na haki za walio wachache ambaye aliuwawa na watawala wa kijeshi wa Naijeria tarehe 10 Novemba, 1995.

Kenya: Mwai Kibaki na Odinga Budi Washirikiane na ICC

  10 Novemba 2009

Ubia wa Kuleta Mabadiliko umetoa tamko linalowataka mwai kibaki na raila odinga kushirikiana na mahakama ya kimataifa ya Jinai na kuhakikisha muswada wa Tume Maalum unapitishwa nchini kenya na kurasimishwa kama sheria ndani ya wiki mbili.

Ghana: Vionjo Sehemu ya Kwanza

  7 Novemba 2009

Sehemu ya kwanza ya vionjo vya Ghana iliyotayarishwa na Gayle: Nchini Ghana, kila kanda ina kitu cha kutoa. Utamaduni, historia, pwani, wanyama na mimea, unaweza ukavivinjari nchini kote, kutokea kwenye mitisitu ya kitropiki kule kusini mpaka mbuga za savana za kaskazini. kama ni mpenzi wa pwani au historia, utaburudika na...

Afrika: Chungu cha Kuiyeyusha Afrika

  5 Novemba 2009

Marvin anaandika kuhusu Afripot, tovuti ya habari inayotilia makini habari za Afrika: “Hivi sasa anatambulisha chungu cha kuyeyushia Afrika – Afripot. Tayari nimo ndani ninayeyuka na ninatumaini kukuona pale na wewe pia kwani mazungumzo kuhusu Afrika na Waafrika yanachukua kasi na kupamba moto. Ni nani ajuaye, inaweza kutengeneza joto la...

Kenya: Ramani Mpya Ya Wazi ya Kitongoji Cha Kibera Kwenye Blogu

  4 Novemba 2009

Mradi wenye lengo la kutengeneza ramani mpya ya wazi ya kitongoji cha Kibera mjini Nairobi, Kenya: “Na jana tulimaliza siku nzima pale MS Action Aid kenya, ambako wanafunzi wa ki-Denmark pamoja na wengine waliotokea kwenye mashirika mbalimbali kama vile Ushahidi, UNICEF, Umande Trust na World Bike, walipoonyeshwa mbinu za kutengeneza...