Habari kuhusu Mauritania kutoka Julai, 2009

Mauritania: Uchaguzi wenye udanganyifu?

  27 Julai 2009

Tarehe 18-07-2009, miezi 11 baada ya mapinduzi ya kijeshi yakiongozwa na Jenerali Mohamed Ould Abdel Aziz, Mauritania imemchagua Jenerali huyu kwa Urais, na kusababisha wapinzani wakuu wa Abdel Aziz kuukataa uchaguzi kwamba ni “kiini macho,” kwa mujibu wa Habari za BBC. Pitio la haraka haraka kwenye blogu za nchi za Saheli linaonyesha kwamba wapinzani wako katika ushirika mzuri.