Habari kuhusu Ethiopia
Jinsi Wanablogu Walifikia Gerezani kwa Kuandika Kuhusu Haki za Binadamu Nchini Ethiopia
Melody Sundberg anachambua uhuru wa kujieleza nchini Ethiopia baada ya wanablogu wa Ethiopia waliokamatwa kukaa siku 100 gerezani: Ethiopia ina idadi ya watu 94,000,000 na ni nchi ya pili yenye wakazi wengi katika bara la Afrika. Hata hivyo, hailingani na mahojiano ya Endalkhachew Chala kupitia Global Voices, kuwa na gazeti...
Dunia Yatwiti Kuwatetea Wanablogu wa ki-Ethiopia Waliokamatwa Julai 31
Unagana na wanablogu wa Global Voices katika zoezi la kutwiti litakalofanyika duniani kote kwa lugha tofauti kuwatetea wanablogu na wanaandishi wa habari wanaokabiliwa na mashtaka ya ugaidi nchini Ethiopia.
Wanablogu wa Zone 9 Washitakiwa kwa Ugaidi Nchini Ethiopia
Wanablogu tisa na waandishi, wanne wao wakiwa wanachama wa Global Voices, wamekana mashitaka yao na wanajiandaa kwa utetezi kesi itakaposikilizw atena Agosti 8.
Umuhimu wa Haki kwa Wanablogu wa Ethiopia
Justice Matters ni blogu inayoripoti kuhusu kesi ya wanablogu wa Zone9 waliokamatwa na waandishi wa habari nchini Ethiopia kwa ajili ya kutoa maoni yao: Blogu hii ina habari zaidi za hivi karibuni kuhusu jitihada za utetezi, ripoti za vyombo vya habari, na hadhi ya kisheria ya wanablogu wa Zone9 nchini...
Je, Madaraka ni Matamu Kiasi cha Watawala wa Afrika Kushindwa Kuyaachia?
Gershom Ndhlovu anaangalia sababu za kwa nini watawala wa Afrika hawataki kuachia madaraka: Kumekuwepo na tetesi, dondoo na hata uvumi kuhusu afya au basi udhaifu wa afya ya Rais wa Zambia Michael Chilufya Sata, aliye madarakani tangu Septemba 2011. Tetesi hizi zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kiasi kwamba serikali...
Ethiopia: #FreeZone9Bloggers Yavuma Kwenye Mtandao wa Tumblr
Global Voices Advocacy ilianzisha mtandao wa Tumblr mapema mwezi Mei kutafuta uungwaji mkono kwa wanablogu tisa na waandishi wa habari – ambao wanne kati yao ni wanachama wa Global Voices – ambao kwa sasa wako kizuizini nchini Ethiopia shauri ya kazi zao. Washirika kutoka duniani kote waliwasilisha picha, ujumbe wa...
Mazungumzo ya GV: Kupigania Kuachiliwa Huru kwa Wanablogu wa Ethiopia wa Zone 9
Wanablogu tisa ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari ---wanne wao wakiwa ni wanachama wa Global Voices ---wanashikiliwa nchini Ethiopia kwa sababu ya kutekeleza majukumu yao. Fahamu namna ya kuunga mkono kampeni ya #FreeZone9Bloggers!
Kwa Nini Kublogu ni Tishio kwa Serikali ya Ethiopia
Beza Tesfaye anaelezea kwa nini kublogu ni tishio kwa serikali ya Ethiopia kufuatia kukamatwa kwa wanablogu tisa Ethiopia: Ninapoandika haya, Kwa uwoga nakumbushwa kwamba nchini Ethiopia, kutoa maoni yako kunaweza kukufanya uakapewa tiketi ya daraja la kwanza gerezani. Kutoka Aprili 25 hadi 26, 2014, wanablogu tisa wa Ethiopia na waandishi...
Ungana na Kampeni ya #FreeZone9Bloggers Twita Mei 14
Ungana na wanablogu wa Global Voices kwa ajili ya kampeni ya kutwiti barani Afrika kwa ajili ya kuunga mkono wanablogu na waandishi wa habari tisa waliokamatwa mwishoni mwa mwezi Aprili na kwa sasa wako rumande nchini Ethiopia.
Njia 4 Unazoweza Kuzitumia Kujiunga na Kampeni ya #FreeZone9Bloggers
Jiunge na kampeni ya kudai kuachiwa kwa wanablogu na waandishi tisa waliokamatwa nchini Ethiopia: Andika barua, tia saini tamko, au andaa tukio kwenye mji wako!