Habari kuhusu Kameruni

Mashoga Washambuliwa Kaskazini mwa Kameruni

  11 Januari 2013

Oscarine Mbozo’a anaripoti [fr] katika blogu ya L'Actu kuwa shoga mmoja akiwa ameambatana na mwenzi wake walizomewa karibu na soko mnamo tarehe 6, Januari 2013, mjini Maroua, Kaskazini mwa Kameruni: Goche Lamine, mfanyabiashara wa madawa, alikamatwa na mwanafunzi wa shule ya sekondari aitwaye Sanda, mwenye umri wa miaka 17. Umati wa...

Global Voices Yashinda Tuzo Ya Highway Africa

  16 Septemba 2012

Timu ya Global Voices inayoandika habari za Nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara imeshinda Tuzo ya Telekom Highway Africa katika kundi la “Blogu bora ya TEHAMA ya Kiafrika”. Mhariri wa Eneo hilo Ndesanjo Macha alikuwepo Afrika Kusini kuipokea tuzo hiyo (na kikombe cha ushindi!) tarehe 11 Sepetemba,...

Cameroon: Ndoto za Umeme kwa Ajili ya Maendeleo ifikapo 2035

  8 Julai 2012

Cameroon inatarajiwa kufikia hadhi ya soko linalokua kwa kasi ifikapo mwaka 2035 kupitia "mafanikio makubwa" ya hatua kwa hatua katika maendeleo ya miundombinu ya usafiri na nishati. Hata hivyo kufikiwa kwa malengo hayo ndani ya muda uliopangwa hakuonekani kuwashawishi wachambuzi wengi wa masuala ya kisiasa, kwa sababu tu changamoto zilziopo ni nyingi.

Suluhisho la Kiradikali la Umaskini Duniani: Ufunguzi wa Mipaka

  4 Januari 2012

Wataalamu kadhaa wanasema kuwa umaskini uliokithiri hauepukiki. Suluhisho la kiradikali zaidi la kupunguza umaskini kwa haraka duniani kwa wataalamu wengi wa uchumi ni kufungua mipaka kati ya nchi na kuruhusu wafanyakazi kuhamia sehemu ambazo nguvukazi inahitajika zaidi.

Kameruni: Wanablogu Waijadili Hotuba ya Obama Ghana

  22 Julai 2009

Rais wa Marekani Barack Obama alitoa hotuba yake Ghana ambayo inaweza kuchukuliwa kuwa kama hotuba ya sera yake ya Afrika. Wakameruni wa nyumbani na wale wa ughaibuni wamekuwa wakijadili maneno yaliyotamkwa na Kiongozi wa Marekani mwenye asili ya Afrika kwa kupitia ulimwengu wa blogu.