Habari kuhusu Tunisia kutoka Januari, 2011
Syria: Propaganda ya Vyombo vya Habari vya Serikali Kuhusu Maandamano ya Tunisia na Misri
Mwanablogu wa ki-Syria Maurice Aaek amegundua[ar] kwamba vyombo vya habari vinavyoendeshwa na serikali nchini Syria vinachapisha habari za uongo na nusu-kweli kuhusu maandamano ya upinzani nchini Tunisia na Misri. Amegundua...
Tunisia: Anonymous Dhidi ya Ammar – Nani Atashinda Vita ya Kuchuja Habari?
Kichuja habari cha Tunisia, kinachojulikana kama Ammar, kinaeendelea kutishia kuziharibu na kuzifunga anuani za wanaharakati wa mtandaoni, katika nchi hiyo ambayo imekuwa ikishuhudia wimbi la maandamano tangu katikati ya mwezi Desemba. Ni leo tu, wanaharakati wamedai kwamba serikali imeingilia anuani zao za barua pepe,na kuziingilia blogu na mitandao yao ya kijamii, na kuzizuia zisifanye kazi. Hatua hii inaonekana kuja kama kulipiza kisasi kwa shambulio lililofanywa na kikundi cha wanaharakati wa mtanda0ni wanaojulikana kama Anonymous, ambalo lililenga njia na mitandao ya muhimu ya Serikali ya Tunisia.