· Machi, 2014

Habari kuhusu Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kutoka Machi, 2014

Video: Usambazaji Vyakula katika Kambi ya Yarmouk-Syria

  5 Machi 2014

Shirika la habari la FAJER liliweka mtandaoni video ya kambi ya wakimbizi ya Yarmouk mjini Damascus wakati wa kupokea mgawo wa chakula cha kuwalisha wakazi 18,000 wa kambi waliobaki, ambao wamelazimishwa kula wanyama waliopotea ili kuokoa maisha yao wakati huu ambapo kuna uhaba mkubwa wa chakula. Video ni ya tarehe...

“Iran haiwezi kuufungia Mtandao wa Facebook Milele”

  4 Machi 2014

Waziri wa Utamaduni na Ulinzi wa Uislamu wa Iran, Ali Jannati, alisema “Iran haiwezi kuufungia Mtandao wa Facebook milele.” Maofisa kadhaa wa Iran kama Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Kigeni, hutumia mitandao ya Twita na Facebook hata wakati tovuti hizo zimefungiwa nchini Iran.

Iran: Mwanafunzi Ahukumiwa Miaka 7 Jela

  4 Machi 2014

Blogu ya PersianBanoo iliripoti kuwa “mwanafunzi mwanaharakati wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Qazvin aliyefukuzwa, Maryam Shafipour amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela. Awali iliripotiwa na familia yake kuwa alikuwa amepigwa na maofisa wa kiume waliokuwa wanamhoji wakati wa kuhojiwa kukiendelea”.