Habari kuhusu Misri

VIDEO: Shairi la Filamu “Maombi ya Woga” Latia Fora Misri

  30 Septemba 2013

Mkusanyiko wa kiraia la Misri Mosireen umekuwa, bila kuchoka, ukiweka kumbukumbuza Mapinduzi ya Januari 25 na matukio yaliyofuata baadae kwa kutumia picha na dokumentari. Moja ya ubunifu wake wa mwisho mwisho ni “Maombi ya Woga”, shairi la filamu iliyotengenezwa na Mahmoud Ezzat na kusimuliwa na mwanachama wa Mosireen Salma Said....

Kubusiana Kwenye Mitaa ya Misri

  15 Septemba 2013

Picha inayosambazwa katika mtandao wa Facebook inayowaonyesha vijana wawili raia wa Misri wakibusiana barabarani iliibua hasira na wengine kuipenda. Ilitolewa na Ahmed ElGohary, mtangazaji aliyepingwa kwa ‘kukosa utu uzima’ kwa sababu ya kuweka picha ya jinsi hiyo. Wengine walisifu uzuri wa picha hiyo na tafsiri yake kwa mapinduzi ya kiutamaduni. Kuonyesha mapenzi hadharanini si jambo linalokubalika nchini...

Makanisa Yashambuliwa Nchini Misri

  22 Agosti 2013

David Degner aweka picha kutoka makanisa yaliyoshambuliwa na kuchomwa katika sehemu iitwayo Mallawi, Minya, Misri ya Juu hapa. Anaandika: Siku ya Ijumaa makanisa mawili katika kijiji cha Mallawi, jimbo la Minya, yalishambuliwa na kuchomwa moto. Baada ya mashambulizi dhidi ya wafuasi wa Morsy  ambapo zaidi ya watu 600 walifariki, wafuasi wa Morsy walikusanyika baada...

PICHA: Makanisa Yanalia Nchini Misri

  22 Agosti 2013

Kufuatia kuchomwa kwa makanisa, msichana mdogo katika Misri ya Juu alichora picha hii iliyonifanya nitiririkwe na machozi: pic.twitter.com/iymw3SF49R — daliaziada (@daliaziada) Agosti 15, 2013 Mtetezi wa haki za wanawake nchini Misri Dalia Aziada aliposti twiti hii  baada ya makanisa kadhaa ya wakristo kuteketezwa katika maeneo mbalimbali nchini Misri kufuatia operesheni ya kikatili  iliyofanywa na jeshi...

Mwana-Habari Menna Alaa Ashambuliwa na Wafuasi wa Morsi

  23 Julai 2013

Mwanablogu na mwanahabari wa video Menna Alaa leo hii ameshambuliwa na waandamanaji wenye hasira wanaomwunga mkono Morsi. Mwanablogu huyo ameweka ushuhuda wake kwa lugha ya kiingereza kwenye makala hii iliyo katika blogu inayokusanya matukio nchini Misri iitwayo Egyptian Chronicles. Anaandika: Kofi nililopigwa usoni, alama iliyobaki usoni mwangu pamoja na kuibwa...

Al Jazeera Yatuhumiwa Kutangaza “Habari za Upendeleo”

  12 Julai 2013

Al Jazeera iko kwenye wakati mgumu nchini Misri kwa kile kinachoelezwa na wengi kuwa ni "upendeleo" wake katika kutangaza habari zake wakati na baada ya kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi mnamo Julai 4. Kituo hicho cha televisheni kilichopo nchini Qatar kinatuhumiwa kuegemea upande wa wafuasi wa Muslim Brotherhood na kimegeuka kuwa mdomo wa kikundi hicho.