· Julai, 2013

Habari kuhusu Misri kutoka Julai, 2013

Mwana-Habari Menna Alaa Ashambuliwa na Wafuasi wa Morsi

  23 Julai 2013

Mwanablogu na mwanahabari wa video Menna Alaa leo hii ameshambuliwa na waandamanaji wenye hasira wanaomwunga mkono Morsi. Mwanablogu huyo ameweka ushuhuda wake kwa lugha ya kiingereza kwenye makala hii iliyo katika blogu inayokusanya matukio nchini Misri iitwayo Egyptian Chronicles. Anaandika: Kofi nililopigwa usoni, alama iliyobaki usoni mwangu pamoja na kuibwa...

Al Jazeera Yatuhumiwa Kutangaza “Habari za Upendeleo”

  12 Julai 2013

Al Jazeera iko kwenye wakati mgumu nchini Misri kwa kile kinachoelezwa na wengi kuwa ni "upendeleo" wake katika kutangaza habari zake wakati na baada ya kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi mnamo Julai 4. Kituo hicho cha televisheni kilichopo nchini Qatar kinatuhumiwa kuegemea upande wa wafuasi wa Muslim Brotherhood na kimegeuka kuwa mdomo wa kikundi hicho.

Misri yasema: “HAYAKUWA mapinduzi ya kijeshi”

  7 Julai 2013

Hatua ya Marekani kuingilia masuala ya ndani ya Misri - habari zinazotangazwa mashirika ya habari, hususani CNN, kuhusu siasa zinavyoendelea Misri - zilikumbana na moto jana usiku. Kung'olewa kwa rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi baada ya kudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja tu madarakani kuliamsha shamra shamra nchi nzima, pamoja na vurugu kati ya wafuasi na wapinzani wa Morsi.

Misri: Wafuasi wa Morsi Wapambana na Waandamanaji Wanaompinga Morsi

  6 Julai 2013

Mapambano yaliyotarajiwa kati ya wafuasi wa Muslim Brotherhood na waandamanaji waliotaka rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi aondoke yametokea leo [June 6, 2013]. Ilikuwa kama mchezo wa kuigiza na ulionekana moja kwa moja kwenye televisheni, na ulirushwa kwa moja kwa moja na vituo vya televisheni vya ndani na vile vya kimataifa. Watu wasiopungua 17 waliuawa na zaidi ya waandamanaji 400 wakijeruhiwa katika mapigano nchini kote Misri leo, tukio ambalo mitandao mingi ya kijamii inalielezea kama "lililotarajiwa" na "linalosikitisha."

Raia wa Misri Wamng'oa Morsi Madarakani

  4 Julai 2013

Mohamed Morsi, ambaye ni kiongozi mkuu wa chama cha Muslim Brotherhood siyo tena Rais wa Misri. Morsi ameondoshwa madarakani baada ya kutumikia kwa mwaka mmoja kama Rais mara baada ya maandamano makubwa nchini kote Misri yaliyomtaka kujiuzulu, maandamano hayo yalianza mapema mwezi Juni 30. Mkuu wa majeshi ya Misri, Generali Abdel Fattah Al Sisi, katika matangazo ya mojakwa moja dakika chache zilizo pita, alisema kuwa, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Katiba ndiye atakayekuwa Rais mpya wa mpito na kwamba serikali ya kitaifa ya Kiteknokrasia itaundwa.

Mwandamanaji Amtaka Morsi Kuondoka Kwa Lugha ya Mafumbo

  3 Julai 2013

Maandamano makubwa ya kumtaka rais wa Misri Mohamed Morsi ajiuzulu yanaendelea nchini Misri kwa siku ya tatu sasa. Kwenye mtandao wa Twita, Assem Memon anaweka picha iliyopigwa kwenye maandamano: @AssemMemon: Bango la Maandamano. Neno ondoka limeandikwa katika lugha 14 za mafumbo. Picha imewekwa kwenye mtandao wa Twita na @ alaafareed pic.twitter.com/S7OOSDfpV6

Misri: Wasalafi Washambulia Makazi ya Washia, Wanne Wauawa

  2 Julai 2013

Watu wanne nchini Misri ambao ni wafuasi wa imani ya Shia wameuawa leo nchini Misri mara baada ya nyumba waliyokuwa wanakutania kushambuliwa na Waislam wenye msimamo mkali, shambulio hili linafuatia wiki mbili za uchochezi dhidi ya waumini wa Shia. Kwa mujibu wa taarifa za awali, nyumba ambayo waumini hao wa Shia waliyoitumia kukutania, iliyopo huko Giza, Cairo, ilishambuliwa na kuchomwa moto. Kwa mujibu wa taarifa za habari za Al Badil, shuhuda mmoja alikaririwa akisema kuwa mmoja wa watu waliouawa alichinjwa na wengine watatu walijeruhiwa vibaya vichwani mwao. Tukio hili la kutisha lilizua ghadhabu kubwa mtandaoni.