Habari kuhusu Venezuela

Venezuela: Tathmini za Baada ya Uchaguzi

  15 Oktoba 2012

Msisimko ulikuwa mkubwa sana usiku wa siku ya Jumapili baada ya matokeo rasmi ya uchaguzi wa Rais wa Venezuela kutangazwa. Sehemu ya nchi ilisherehekea kuendelezwa kwa 'Mapinduzi ya Venezuela' chini ya Rais Hugo Chávez, wakati upande mwingine ulilalamika kwa kushindwa tena kwenye uchaguzi huo.

Venezuela: Ni Chávez Tena kwa Miaka Sita Zaidi

  11 Oktoba 2012

Baada ya chaguzi zilizokuwa na changamoto na ushindani mkubwa katika muongo uliopita, Venezuela itaongeza miaka mingine sita kwa utawala wa Hugo Chávez Frías ulioanza mwaka 1999. Idadi ya watu waliokuwa mtandaoni hasa kwenye mitandao ya kijamii, hasusani twita, ilikuwa kubwa sana hasa kabla matokeo rasmi hayajatangazwa.

Venezuela: Picha za Siku ya Uchaguzi

Leo, mitandao ya kijamii nchini Venezuela inatoa taswira ya nchi hiyo kuwa ukingoni mwa zoezi muhimu. Pamoja na shuhuda mbalimbali, taarifa, tetesi na mapendekezo, majukwaa ya vyombo vya habari vya kijamii kama vile Twita, Facebook na Flickr yameonyesha picha zinazoonyesha ushiriki mkubwa wa watu katika kumchagua Rais ajaye wa Jamuhuri hiyo.

Venezuela: ‘Sura na Sauti’ za Uchaguzi

  8 Oktoba 2012

Kwa kutumia mfululizo wa picha na nukuu, mpiga picha wa Kireno Eduardo Leal anayateka mawazo na hisia za watu wa Venezuela kwa jinsi zinavyoeleza watakuwa wanampigia nani kura kuwa Rais katika uchaguzi uliofanyika Jumapili ya Oktoba 7.Kwa kutumia mfululizo wa picha na nukuu, mpiga picha wa Kireno Eduardo Leal anayateka mawazo na hisia za watu wa Venezuela kwa jinsi zinavyoeleza watakuwa wanampigia nani kura kuwa Rais katika uchaguzi uliofanyika Jumapili ya Oktoba 7.

Venezuela: Ziara ya Mahmoud Ahmadinejad Yaibua Utata

  25 Januari 2012

Rais wa Iran, Mahmud Ahmadinejad, aliwasili nchini Venezuela Jumapili, Januari 8, katika kituo chake cha kwanza cha ziara ya ya nchi kadhaa za Marekani ya Kusini. Ziara yake imechochea miitiko mikali kweny mitandao ya kijamii, ambako watumiaji wanahoji kama uwepo wake unaweza kuwa na faida yoyote kwa taifa.

Venezuela: Mwanaharakati wa mtandaoni Luis Carlos Díaz anyanyaswa na kutishwa na “wezi wa akaunti za mtandaoni”

Kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha miezi minne tu, mwandishi wa habari wa Venezuela na mwanaharakati, Luis Luis Carlos Díaz, amenyanyaswa kupitia akaunti yake ya Twita [1] na simu yake ya mkononi na kikundi kinachojulikana kama cha "wezi wa akaunti za mtandaoni", na ambao hutumia jina la N33 [2], na bila shaka ni kundi lilelile la watu ambao miezi michache iliyopita liliiba maneno ya siri ya akaunti za Twita na baruapepe ya karibu watu thelathini maarufu wa Venezuela, baadhi yao ni waandishi wa habari Sebastiana Barráez, Ibéyise Pacheco, mchekeshaji wa kisiasa Laureano Márquez, mwanaharakati Rocío San Miguel na mwandishi Leonardo Padrón, miongoni mwa wengine wengi.

Venezuela: Wahindi wa Yukpa, Chavez na Mgogoro wa Ardhi

  6 Septemba 2008

Picha za video zinazotumwa kwenye mtandao wa internet na vyombo vya habari vya kiraia zinaonyesha yale yanayojiri kuhusu mgogoro unaoibuka nchini Venezuela kati ya Wahindi wa jamii ya Yukpa wanaoishi katika milima ya Perijá, wamiliki wa ardhi na Rais Chávez. Mgogoro huu kuhusu mipaka ya ardhi umekuwapo kwa takribani miaka 30, yaani tangu pale vikosi vya jeshi vilipowandoa kwa nguvu wanajamii wenyeji ya Ki-Yukpa na kuwapa ardhi hiyo wamiliki wapya walioanzisha mashamba makubwa ya mifugo, hasa ng'ombe, ambao wameendelea kuitumia ardhi hiyo tangu wakati huo.