Habari kuhusu Colombia

Matatizo ya Colombia kwa Ukosefu wa Usawa Mijini

  11 Novemba 2013

Taarifa ya utafiti wa hivi karibuni wa Umoja wa Mataifailiyoripotiwa katika El Tiempo, iligundua kwamba Colombia ilikuwa nchi ambayo iliongezeka kwa wingi wa kukosekana kwa usawa wa mijini mwake kwa miongo miwili iliyopita.Bogotá ilikuwa kanda isiyo na usawa kwa mji mkuu. Na kwa miji 13 ya Colombia iliyosomwa na Umoja...

Colombia: Mwanahabari Raia Atishwa Kuhusu Video Iliyoenea

  25 Februari 2012

Mwanahabari raia Bladimir Sánchez ameshapata vitisho kwa maisha yake kwa kueneza video inayoonhesha kuhamishwa kwa fujo kwa wakulima na wavuvi wanaopinga ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme katika eneo la Huila, nchini Colombia. Baada ya muda usiozidi siku tatu, watu zaidi ya 600,000 wameitazama.

Colombia: Mockus na Fajardo Waungana kwa Ajili ya Uchaguzi wa Rais

  24 Aprili 2010

Mameya wawili wa zamani wa amajiji 2 makubwa zaidi nchini Kolombia wameunganisha majeshi kugombea katika uchaguzi wa rais wa Mei 30 kwa tiketi moja. Umoja huu mpya wa Chama cha Kijani umepokewa vizuri na watumiaji wa vyombo vya habari vya kijamii, ambo ni sehemu kubwa ya mkakati wa kampeni.

Colombia: Ugumu wa Kutofautisha Wazuri na Wabaya

  23 Januari 2010

Kwa kupitia upigaji video wa kiraia, asasi tofauti nchini Colombia zinatoa mitazamo yao kuhusu uhalifu, unyama na migogoro inayohusisha matumizi ya silaha, ambayo ni vigumu kuwatofautisha watu wazuri kutoka kwa wabaya.

Colombia: Watu Wanaswa na Mitego ya Upatu

  14 Septemba 2008

Kwa kupitia picha za video na mtandao wa marafiki wa Facebook, raia wa Colombia, Diego Alejandro, anaweka wazi udanganyifu na utapeli mkubwa uliojificha nyuma ya michezo ya upatu ambayo inatangazwa kama njia mbadala za uwekezaji. Katika nchi ambapo akaunti za benki zimepoteza maana kwa sababu ada za uendeshaji ziko juu kuliko riba anayopata mwenye akaunti, michezo hii ya upatu inayoshawishi kumjaza mtu mapesa, ambapo raia wanalipa kiasi fulani cha pesa ili kujiunga na kisha kuingiza marafiki zao 7 kabla wao hawajaanza kufurahia riba ya juu ajabu (kati ya asilimia 40 mpaka 70) basi imekuwa ni kivutio kikubwa mno.