Habari kuhusu Ukraine

Mazungumzo ya GV: Kipi Kinafuata Nchini Ukraine?

  7 Machi 2014

Kipi kinafuata kwenye vuguvugu la maaandamano ya Ukraine? Maandamano na umwagaji damu ulisababisha kung'oka kwa rais anayetuhumiwa kuwa fisadi. Lakini sasa, wakati Urusi ikijiandaa kijeshi na Crimea ikifikiria kujitenga, yapo maswali mengi yasiyoisha kuhusu mustakabali wa kisiasa nchini Ukraine pamoja na uhusiano wake na Umoja wa Ulaya.

Matukio ya Ghasia Zinazofanywa na Majeshi ya Urusi nchini Ukraine

  4 Machi 2014

Blogu maarufu ya “Tafsiri za Maida ilichapisha bandiko la mtandao wa Facebook la Dmitry Tymchuk, Mkuu wa Kituo cha Ukraine cha Stadi za Siasa za Kijeshi, linaloeleza matukio ya ghasia za kimataifa zinazodaiwa kufanyika na “matendo yasiyo ya kawaida” tangu Februari 2014. Tymchuk anaanza uchambuzi huu kwa kusema: Kwa mfano,...

Rais Yanukovych wa Ukraine ang'olewa madarakani

  24 Februari 2014

Baada ya maandamano, vurugu na upinzani dhidi ya serikali uliosababisha vifo vya watu wapatao 100, Bunge la Ukraine hatimaye limepiga kura ya kumwondoa Rais Viktor Yanukovych kama hatua ya kujibu shinikizo la waandamanaji. Tayari Rais Yanukovych amenukuliwa akisema hana mpango wa kutoroka nchi. Soma zaidi kupitia kiungo hiki [en]

Wabunge wa Ukraine Wataka Utoaji Mimba Upigwe Marufuku Kisheria

  4 Mei 2013

Mapema mwezi Aprili, Wabunge watatu kutoka kambi ya Upinzani iitwayo“Svoboda” walipeleka mswada bungeni wenye lengo la kupiga marufuku utoaji mimba nchini Ukraine. Tetyana Bohdanova anataarifu mwitikio wa watumiaji wa mtandao kufuatia hatua hii ya Bunge la Ukraine.