Habari kuhusu Urusi kutoka Oktoba, 2016
Kashfa Nyingine Yalikumba Kanisa la Orthodox la Nchini Urusi Kufuatia Kasisi Kuonekana na Saa Yenye Thamani ya $40,000
Kanisa la Orthodox la nchini Urusi limejikuta katika kashfa kwa mara nyingine, na kwa sasa kashfa hii inahusishwa na saa ya mkononi ya Kasisi mwandamizi wa St. Petersburg.
Picha za Mtandao wa Instagram Zaonesha Ukungu Unavyoifunika Khabarovsk
Wakazi wa Khabarovsk, mji ulioko Mashariki ya Mbali nchini Urusi, wamekuwa wakikaa ndani au kulazimika kuficha nyuso zao wanapokwenda nje tangu ukungu mzito kuufunika mji wao tangu Jumanne.
Urusi Inadaiwa Kuwa na Mpango wa Kuufungia Mtandao wa LinkedIn
LinkedIn, mtandao mkubwa zaidi unaowaunganisha wataalaam duniani kote, uko hatarini kufungiwa nchini Urusi, ambako wapelelezi wa serikali wamefanikiwa kuishawishi mahakama moja mjini Moscow kuufungia mtandao huo.
Kilichoandikwa na Shirika la Habari Urusi Wakati wa Mdahalo wa Mwisho wa Urais Marekani
Mradi wa RuNet unaoangazia habari za Urusi unapitia twiti zilizoandikwa usiku wa mdahalo huo na shirika kubwa la habari la Urusi ili kupata picha ya kile kilichoendelea jijini Moscow.
Yaliyojiri Wiki Hii Hapa Global Voices: Anahitaji Kutendewa Haki
Wiki hii, tunakuletea wanawake wanaosaka au wanaopata haki zao nchini Poland, Uruguay, Urusi na Syria.