Habari kuhusu Urusi kutoka Aprili, 2013
Urusi: Wapinzani Wapumbazwa na Uchaguzi wa Awali, Wapoteza Uchaguzi Halisi
Mwezi Agosti (mwaka 2012), Mtandao wa Sauti za Dunia uliripoti habari za wanaharakati kadhaa wanaohusika na vuguvugu la maandamano nchini Urusi wanaogombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Walitumaini itakuwa rahisi kushinda uchaguzi huo mdogo, ambao ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Oktoba 14, 2012 huku idadi ya ndogo ya wapiga kura wakiojitokeza tena ndani ya madai ya siku nyingi ya wizi wa kura katika uchaguzi, Warusi walishiriki kwa maelfu katika uchaguzi nchini kote, kupiga kura kuwachagua mameya wa miji, madiwani, na wabunge wa mikoa.
Asasi za Kiraia za Urusi “Zakaguliwa” na Mwendesha Mashitaka
Wanaharakati wa DemVybor katika jiji kuu la eneo la Voronezh waliripoti kwenye blogu ya DemVybor[ru] kwamba Asasi Zisizo ki-Serikali zinakaguliwa na ofisi ya mwendesha mashitaka wa umma wa jiji hilo. Mashirika...