Habari kuhusu Ulaya Mashariki na Kati
Yaliyojiri Wiki Hii Global Voices: Yeyote ni Kipaumbele?
Wiki hii tunakupeleka hadi China, Mexico, Jamaica, Macedonia na Uganda, ambapo tunaongea na Prudence Nyamishana ambaye anatusimulia ni kwa nini Raia wa Uganda hawakufurahishwa na vipaumbele vya serikali yao.
Yaliyojiri Wiki Hili Global Voices: ‘Nyaraka za Panama’ ni Kitu Gani?
Katika kipidni hiki, hedhi zatumika kisiasa nchini Poland, wa-Chile wenye asili ya Afrika wadai kutambuliwa nchini Chile, na wadhibiti mtandao nchini China wanafanya juhudi za kuondoa nyaraka za Panama -- hata ikibidi kwenye barua pepe.
Umesikia? Podikasti ya Global Voices Imerejea
Baada ya likizo ya miaka mitatu, Podikasti ya Global Voices imerejea. Katika toleo hili, tunakupeleka Mexico, China, Tajikistan, Macedonia and Russia.
Kilichotokea Mbwa ‘Mjamzito’ Alipozikwa Hai huko Voronezh
Serikali ya mtaa iliposhindwa kujibu ombi la msaada, watu kadhaa waliamua kujichukulia hatua, kuondoa matofali na kuchimba kumwokoa mbwa huyo aliyekuwa amebanwa.
Hivi Ndivyo Chechen Inavyokabiliana na Kundi la ISIS
Video ya Kadyrov ikiwaonesha wanaume wa Chechen waliokamatwa kwa kushawishi watu kupitia mitandao ya kijamii ili wajiunge na kundi la ISIS, na wazee wanaoonekana wakiwakaripia ni ndugu zao pamoja na viongozi wa eneo wanaloishi wanaume hao
Raia wa Masedonia Watumia Sheria ya Uhuru wa Habari Kupinga Sheria Mpya ya Wafanyakazi
Baadhi ya wafanyakazi wasio na mikataba y kudumu pamoja na wale walio na mwajiri zaidi ya mmoja walizuiwa kupokea mishahara yao ya mwezi Januari kwa mujibu wa sheria mpya za kodi na utoaji wa ada. Waandamani wana lengo la kuweka bayana namna serikali isivyokuwa na utaratibu mzuri wa kutekeleza sheria hizi.
Serikali ya Masedonia Yazuia Kupiga Picha za Maandamano kwa Kutumia Kamera za Anga
Video na picha zilizotengenezwa kwa kutumia kamera inayopaa angani zilikuwa nyenzo muhimu ya kuonesha ukubwa wa maandamano ya wanafunzi, ambayo yameitwa maandamano makubwa ya wanafunzi kuwahi kutokea nchini Masedonia tangu uhuru.
Pamoja na Wapiga Kura Kutilia Shaka Sera Zake, Croatia Yapata Rais Mwanamke
Croatia ipo katika mpasuko mkubwa wa kisiasa. Kolinda Grabar Kitarović ameweza kunyakua kiti cha uRais kufuati ushindi mwembamba alioupata dhidi ya Rais anayemaliza muda wake, Ivo Jospović katika duru ya pili ya uchaguzi uliofanyika mwezi Januari, 2015 kwa kupata asilimia 50.74 ya kura zote.
Vyombo vya Habari Vyaususia Wimbo wa Kupigania Uhuru Ulioimbwa na Msanii Maarufu Nchini Macedonia
Msanii maarufu wa Macedonia wa miondoko ya kufoka foka amejikuta akipoteza umaarufu baada ya kuachia ‘kibao’ kinachojadili masuala ya uhuru wa habari nchini Macedonia.
Alama ya Utambulisho wa Kompyuta ya Serikali ya Urusi Yakamatwa Ikihariri Makala ya Wikipedia ya Ndege ya MH17
Alama kadhaa za utambulisho wa kompyuta (IP address) ndani ya serikali ya Urusi zimeendelea kufanya kazi kazi kwenye kamusi elezo ya Wikipedia, ambapo kompyuta ya Shirika la Upelelezi la Urusi, FSO, ilihariri makala ya Kijerumani kuhusu Ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia MH17, ikibadili neno “wanaotaka kujitenga” kuwa “waasi.” Teknolojia ya...