Habari kuhusu Ulaya Mashariki na Kati kutoka Januari, 2010
Slovakia, Hungaria: Heri ya Mwaka Mpya!
Uhusiano kati ya nchi mbili jirani za Slovakia na Hungaria ulianza kutetereka katika mwaka uliopita - lakini baadhi ya wananchi wa Slovakia na Hungaria wanafanya juhudi kurekebisha hali hiyo kwa kuzindua kampeni ya mtandaoni inayojulikana kama "Štastný nový rok, Slovensko! / Boldog Új Évet Magyarország!" ("Heri ya Mwaka Mpya, Slovakia!/Heri ya Mwaka Mpya, Hungaria!).