Habari kuhusu Trinidad na Tobago

Trinidad na Tobago: Tume ya Mapinduzi

  18 Machi 2014

Je, Trinis inajali ripoti ya dat de iliyotolewa na Tume ya kuchunguza jaribio la mapinduzi ya Abu Bakr mwaka 1990 ambayo ndio kwanza imetoka? Trini inapendekeza kwamba kutolewa kwa matokeo haya kunaweza kuchukuliwa kuwa ni ya kiwango cha chini, na yamekuja kwa kuchelewa.

Trinidad na Tobago: Kati ya Serikali Mbili

  3 Machi 2014

Katika mukhtadha wa idadi na ukubwa wa miradi inayotekelezwa kwa kupitia mipango ya serikali ya nchi hiyo, Afra Raymond anaeleza kwa nini ushirika wa kiwango cha juu unaoonyeshwa hivi sasa na Trinidad na Tobago kwa China ni “suala nyeti linalostahili tafakuri ya kina.”

Caribbean: Kwaheri, Nelson Mandela

  10 Disemba 2013

Tangazo la kifo cha Nelson Mandela limepokelewa kwa mshtuko. Wanablogu wa maeneo mbalimbali wanashirikishana mawazo yao kuhusu kuondoka kwa mmoja wa magwiji wa upinzani kwa njia za amani duniani aliyetutoka.

Trinidad na Tobago: Ufisadi na Utawala wa Sheria

  9 Oktoba 2012

Hivi karibuni, masuala ya utawala wa sheria yamekuwa yamekuwa yakitawala serikali iliyoko madarakani. Kwa kuwa na kipengere cha 34 ambacho hakifahamiki sana miongoni mwa wananchi, hali ya mambo imebadilika na kuwa utawala wa kiimla, na […] tunaweza kuona ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka yamebadilisha kabisa tabia za wale tuliowaona...

Barbados, Trinidad & Tobago:Plastiki na Uchafuzi wa Mazingira

  15 Disemba 2009

“Fanya matembezi kwenye pwani yoyote nchini Barbados – na utaona uchafu wa plastiki uliosukumwa ufukweni”: Barbados Free Press anauliza kama uuzaji wa chupa za plastiki za maji uwekewe vikwazo, wakati Mtrinidadi Keith Francis pia anaguswa na suala la uchafuzi wa mazingira kwa plastiki ulimwenguni.

Trinidad & Tobago: Kampeni ya 350

  26 Oktoba 2009

“Trinidad na Tobago ni kisiwa tajiri na nchi inayoendelea tajiri kwa mafuta na gesi asilia. Lakini pia tunashuhudia madhara mabaya ya maendeleo ya haraka kwenye nyanja za viwanda katika visiwa vyetu. Hii ni fursa ya sauti za wanawake kusikika”: Attillah Springer anajihusisha na kampeni ya hali ya hewa 350.

Trinidad & Tobago: Mtrini Mpaka Kwenye Mifupa?

  24 Oktoba 2009

“Kila siku ambayo ninapitia habari ninazidi kushawishika kuwa ninataka kuachana na klabu ya ‘Mimi ni Mtrini’ na kwenda sehemu nyingine”: Coffeewallah ameshachoka na kila kitu kuanzia uhalifu mpaka kodi.