· Februari, 2009

Habari kuhusu Nchi za Caribiani kutoka Februari, 2009

Martinique: Uhuru na “Ubeberu” wa Kifaransa

  26 Februari 2009

Wakati harakati za wafanyakazi zinaendelea huko Martinique na Guadeloupe, wanablogu wa Martinique wanapima uhuru wa Idara za Ng'ambo utamaanisha nini. Le blog de [moi] anaona dhana ya kuwa Martinique haiwezi kujitegemea ni dhana inayotusi na ya kibeberu. Wasomaji wake wanadhani kuwa ukweli wa kisiwa chochote kidogo ni kuwa kila siku kitakuwa katika kivuli cha wengine.

Guadeloupe: Hali Tete Yazua Ghasia

  26 Februari 2009

Baada ya wiki za maandamano ya amani katika Idara za Ng'ambo za Ufaransa za Guadeloupe na Martinique, mambo yaligeuka na kuwa ghasia siku ya jumatatu, polisi na waandamanaji walipambana katika jiji kubwa la Guadeloupe, Pointe-a-Pitre. Wafanyakazi wanapinga ukosefu wa ajira unaoongezeka pamoja na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu, ambazo nyingi zake huagizwa kutoka Ufaransa.

Haiti: Fanmi Lavalas na Uchaguzi Ujao

  15 Februari 2009

Mwishoni mwa juma lililopita, ulimwengu wa wanablogu wa Kihaiti ulijaa habari za kutengwa kwa vyama vya siasa na Tume ya Muda ya Uchaguzi kwenye uchaguzi wa maseneta utakaofanyika mwezi Aprili 2009 , na siku ya tarehe 6 Januari, tume hiyo CEP ilichapisha orodha ya wagombea ubunge watakaokwaana kwenye uchaguzi ujao wa bunge nchini Haiti. Wanablogu wanaandika mawazo yao kuhusu wagombea walioachwa.