Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Aprili, 2014
Utafiti wa Wenyeji katika Chuo cha Bahamas
Akifuatilia posti yake kuhusu “ujinga wa kupunguza bajeti kwa Chuo cha Bahamas”, Blogworld anasema: Si tu kwamba chuo hicho ni taasisi ya taifa ya elimu ya juu, lakini ndio taasisi pekee ya umma kwa wenyeji ambayo inahusiana na aina yoyote ya utafiti unaoendelea katika nchi ya Bahama.
VIDEO: Wimbo wa ‘Furaha’ wa Pharrell Williams na Taswira Halisi ya El Salvador
Wananchi wa Salvador wametengeneza toleo lao la wimbo “Happy” [furaha] ulioimbwa na Pharrell Williams. Mwanablogu Mildred Largaespada anaisifu video hiyo kwenye ukurasa wake wa Facebook [es]: ni nzuri. Na ndiyo, kama ilivyo kwenye maisha halisi, video hii ni halisi: wakati mwingi wa siku, wanawake na wanaume wa El Salvador wanaoneka...
Urabuni: Hijab na Ubaguzi wa Kimagharibi
Mwanablogu wa Mirsi Nadia El Awady anaandika posti ya blogu yake ambapo anahoji kama wanawake wanaovaa Hijabu wanabaduliwa kwenye nchi za magharibi ama la. Nadia, kama Mmisri alikulia Marekani na ameishi kwa kipindi kirefu Ulaya, anaelezea uzoefu wake kuhusu mwitikio alioupata kwenye nchi za Mashariki na Magharibi linapokuja suala la...
Amnesty International: ‘Mfululizo wa Ghasia ni Tishio la Utawala wa Sheria Nchini Venezuela’
Shirika la kutetea haki za binadamu, Amnesty International limetoa taarifa inayo weka kumbukumbu sawa “kuhusu madai ya uvunjifu wa haki za bindamu na unyanyasaji uliofanywa katika mukhtadha wa maadamano makubwa ya umma tangu mwezi Februari.” “Nchi hiyo iko kwenye hatari ya kuwa na mfululizo wa matukio ya ghasia kama hatua...
Utani Mitandaoni: Siku ya Wajinga Nchini Ethiopia
Wa-Ethiopia kwenye mtandao wa twita wanasherehekea siku ya wajinga duniani kwa kutangaza habari bandia ambazo zinaiga uongo unaotangazwa na vyombo vya habari vya serikali. Raia mmoja wa Ethiopia anayetwiti: “Wanatangaza uongo wa mchana siku 365 za mwaka, ngoja twarudishie dozi ya kuwatosha yenye habari za uongo kadri tunavyoweza”. Wafuatilie ili...