Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Aprili, 2014
Video Inayoonyesha jinsi Marekani Iliangusha Mabomu ya Tani Milioni 2.5 Nchini Laos
Mother Jones alipakia video ambayo inaiga utupaji mabomu 600 uliofanywa na Marekani nchini Laos kati ya mwaka wa 1965 hadi 1973 wakati wa zama za Vita ya Vietnam.
PICHA: Maandamano mjini Caracas, Aprili 1
Tovuti ya PRODAVINCI inachapisha picha nne za Andrés Kerese zilizopigwa wakati wa maandamano yaliyotokea Chacao, moja ya mitaa ya wilaya ya Caracas, Jumanne, Aprili 1, 2014.
Mradi Wa Kutumia Simu za Mkononi Kuhamasisha Usomaji
Lauri anaandika kuhusu mradi uliopo Afrika Kusini, Mfuko wa Usomaji wa FunDza, unaotumia teknolojia ya simu za mkononi kuhamasisha tabia ya kusoma kwa watoto: Kinachofurahisha, hata hivyo, ni pale Waafrika wanapopata majibu ya kiubinifu kwa matatizo yao. Mradi wa FunDza ni mfano moja wapo. Simu za mkononi zimeenea sana nchini...
“Ni wa Kike!”: Kampeni ya Kukomesha Utoaji wa “Mimba za Kike” Nchini India na China
Tovuti ya MujeresMundi, inayoongozwa na mtaalamu wa mawasiliano anayeishi Peru na Ubelgiji Xaviera Medina, inahusika na kampeni ya kuelemisha watu kuhusu “Ni mtoto wa Kike” inakosudiwa kukomesha utoaji wa mimba za kike nchini India na China: Wasichana wanauawa mithili ya mauaji ya kimbari ya jinsia katika muongo mmoja kuliko watu...
Shirika la Friedrich Ebert Lachapisha Ripoti ya Matumizi ya Mitandao ya Kijamii Nchini Cameroon
Shirika la Friedrich Ebert limechapisha ripoti ya utafiti kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii nchini Cameroon: Kwa kiwango kipi, kwa malengo yapi na kwa akina nani basi mitandao ya kijamii kama Twita, Facebook, Blogu, Linkedin, nk. inatumika nchini humo? Kujua majibu ya maswali hayo, Shirika la Friedrich Ebert limetoa taarifa...
Kwa Nini Rais wa Madagaska Hajatangaza Uteuzi wa Waziri Mkuu
Rais mpya wa Madagaska Hery Rajaonarimampianina alichaguliwa kuwa raia mnamo Desemba 20, 2013. Miezi michache baadae, bado hajatangaza uteuzi wa waziri mkuu wa serikali yake mpya. Wachunguzi wengi wanashangaa kwa nini imechukua muda mrefu. Mwanablogu wa Kimalagasi Michael Rakotoarison ana maoni tofauti kuhusiana na hali hiyo; hoja yake ni kuwa huenda...
Kwa nini Rwanda Inaituhumu Ufaransa Kusaidia Mauaji ya Kimbari ya 1994
Wakati Rwanda ikiwakumbuka waathirika wa mauaji ya kimbari yalitokea miaka 20 iliyopita, Rais Kagame anasema tena kuwa Ufaransa lazima “ikabiliane na ukweli mgumu” wa kukiri kushiriki kwenye mauaji hayo ya mwaka 1994 [fr]. Kama matokeo ya matamshi hayo, serikali ya Ufaransa imesusia matukio yote ya kukumbuka mauaji hayo na waziri...
Uchaguzi Mkuu wa India 2014: Kampeni Kwenye Mitandao ya Kijamii
Mitandao ya kijamii imekuwa ni sehemu ya ugunduzi na ubunifu. Milind Deora [Waziri wa Muungano na Mbunge wa Mumbai Kusini] anatamba kuwa mgombea wa kwanza kupatikana kwa wapiga kura wake kwenye mtandao wa WhatsApp na BBM, na huko anajadili mpango kazi wake ikiwa ni pamoja na shughuli zake na mipango...
Hadithi ya Mapenzi Kibera
Hii ni hadithi ya kusisimua ya mapenzi kati ya Sam, anayetoka Kibera, makazi ya masikini kwenye jiji la Nairobi, Kenya, na Alissa, anayetoka Minnesota, Marekani: Bila shaka, hii ni hadithi ya mapenzi isiyo na kifani mwaka huu!!! Alissa anatoka Minnesota, huko Sam alizaliwa na kulelewa Kibera. Ilikuwaje ‘njiwa hawa wa...
Jiunge na IGF Japan Kujadili Utawala wa Mtandao
IGF Japan, hatua ya maendeleo nchini Japani ya Jukwaa la Utawala Mtandao, ambapo watu wanaojihusisha mtandaoni huja pamoja kujadili changamoto za utawala wa mtandao, ulifanyika Machi 14, 2014