· Machi, 2014

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Machi, 2014

Trinidad na Tobago: Washindi wa Tuzo za Hollick Arvon

  20 Machi 2014

Blogu ya Bocas Lit Fest imewatangaza waandishi chipukizi kutoka Jamaica, Grenada, St. Vincent na Trinidad na Tobago kuwa washindi wa Tuzo zinazovuta watu wengi za Waandishi wa nchi za Karibiani za Hollick Arvon kwa mwaka 2014, ambazo kwa mwaka huu zilifanyika kwa mara ya pili.

Je, Sheria Mpya ya Ubakaji India Inawasaidia Wanawake?

  20 Machi 2014

Tumepata sheria ambayo inaelekeza kuadhibu ubakaji, na ambayo imebanua tafsiri ya ubakaji na kujumuisha watu wengi zaidi – wakati tatizo kubwa lilikuwa kwamba watu waliokuwa wanabakwa kwa mujibu wa tafsiri na adhabu za zamani hawakuwa wanatendewa haki katika nchi ambayo kuna ubakaji kw akila dakika saba, lakini hakuna hata tukio...

Trinidad na Tobago: Tume ya Mapinduzi

  18 Machi 2014

Je, Trinis inajali ripoti ya dat de iliyotolewa na Tume ya kuchunguza jaribio la mapinduzi ya Abu Bakr mwaka 1990 ambayo ndio kwanza imetoka? Trini inapendekeza kwamba kutolewa kwa matokeo haya kunaweza kuchukuliwa kuwa ni ya kiwango cha chini, na yamekuja kwa kuchelewa.

Namna Tabia ya Kula Hotelini Inavyoathiri Utamaduni wa Kula Mtaani Indonesia

Ismanto kutoka Yogyakarta nchini Indonesia anabainisha namna mtindo mpya wa kimagharibi wa kula mikahawani unapunguza tabia ya kula “vyakula vya kufunikwa na plastiki” inayofahamika kama ‘angkringan': … vyakula vya angkringan vimepungua. Wanafunzi hawazitumii tena, wakifurahia kulipia vyakula ghali bei iliyo mara mbili zaidi, kunywa na kujumuika na watu katika mtindo...

Korea Kaskazini: Ni Lini Itaanguka?

  15 Machi 2014

Ingawa Korea Kusini inaonekana kutengeneza mahusiano na Korea ya Kaskazini, wataalamu wana wasiwasi kidogo kuhusu kubashiri kuanguka kwa Korea Kaskazini. NKnews.org ilichapisha posti nzuri kuhusu uwezekano wa kutawanyika kwa utawala wa kidikteta, akihitimisha kuwa ‘mageuzi ya kiuchumi ya Pyongyang yanaongeza uwezekano wa tukio la kuanguka vibaya’.

Teknolojia ya Kiafrika: Mradi wa TechAfrique Watathmini Hatua Iliyofikiwa

 Le continent africain apparaît comme la nouvelle frontière mondiale du développement numérique. Ce développement provoque une nouvelle impulsion entrepreneuriale en Afrique, et notamment en Afrique francophone. Mais ce potentiel reste très largement méconnu en Europe ainsi qu'en France.  Bara la Afrika linaonekana kuwa kiongozi mpya wa dunia katika maendeleo ya kidijitali. Maendeleo haya yamesababisha kukua kwa ujasiria...

Kuhusu habari zetu za Muhtasari wa Habari

Hizi ni habari mpya zilizoandikwa kwa muhtasari.