Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Septemba, 2013
Vyombo vya Habari vya Magharibi na Taswira ya Ellen Sirleaf Johnson
Aaron Leaf anajadili jinsi taswira ya rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, hujengwa na vyombo vya habari kimagharibi kama alama ya mambo yote mazuri. Anasema kwamba hili ndiyo simulizi lililomwezesha Sirleaf kuwa mhimili wa maendeleo ya kimataifa na uwezeshaji wa wanawake.
Kubusiana Kwenye Mitaa ya Misri
Picha inayosambazwa katika mtandao wa Facebook inayowaonyesha vijana wawili raia wa Misri wakibusiana barabarani iliibua hasira na wengine kuipenda. Ilitolewa na Ahmed ElGohary, mtangazaji aliyepingwa kwa ‘kukosa utu uzima’ kwa sababu ya kuweka picha ya jinsi hiyo. Wengine walisifu uzuri wa picha hiyo na tafsiri yake kwa mapinduzi ya kiutamaduni. Kuonyesha mapenzi hadharanini si jambo linalokubalika nchini...
Iran: “Mauaji” ya Wapinzani wa Iran 52 Wasiokuwa na Silaha
Vikosi vya usalama vya Iraq vilifanya “mauaji” ya wapinzani wa Iran wapatao 52 ambao hata hivyo hawakuwa na silaha asubuhi ya Jumapili ndani ya kambi yao kaskazini mwa Baghdad, mujahedeen-e-Khalq, wafungwa wa Iran walisema. Netizens in Balatarin, tovuti maarufu ya kusambaza habarii, iliweka picha kadhaa, filamu na posti kuhusiana na shambulio...
Peru: Wafanyabiashara Wachoma Nguo Kupinga Bidhaa za Kichina
Wafanyabiashara kutoka eneo la Gamarra [es], kituo maarufu cha viwanda vya nguo na ambako ndiko lilipo eneo la kibiashara jijini Lima, walichoma nguo zilizoingizwa kutoka China [es] katika mitaa kupinga biashara hiyo ya nguo zinazouzwa bei ndogo ambazo, kwa mujibu wao, hufanya biashara zao kufilisika. Kwenye mtandao wa Twita, Alfredo “Alial” (@ Alfredo_jch) [es] alipendekeza...