Habari kutoka Muhtasari wa Habari na Marekani ya Kaskazini
Serikali ya Marekani Yadai Takwimu za Shirika la Indymedia Athens
Mnamo Septemba 5, Wizara ya Sheria ya Marekani iliitaka shirika linaloshughulika na masuala ya kuhifadhi tovuti iitwayo May First kutoa taarifa za mmoja wa wateja wake, ambaye ni Kituo cha Ugiriki cha cha Uandishi Huru Athens, kinachofahamika kama Indymedia Athens. Likiwa limeanzishwa mwaka 2005, May First ni shirika lisilo la kibiashara linalojikita...
Video ya Dakika 5, Yaweza Kuwa Tiketi Yako ya Kwenda Mjini New York
Muungano wa Ustaarabu wa Umoja wa Mataifa (UNAOC) inawaalika vijana chini ya umri wa miaka 25 kuwasilisha video walizozitengeneza wenyewe zenye urefu wa dakika 5 juu ya uhamiaji, tofauti na kuingizwa kijamii kwa ajili ya tamasha kubwa la filamu 2014. Video tatu zitakazoshinda zitazawadiwa Dola za Marekani 1000 na watengenezaji...
Hadithi ya Mapenzi Kibera
Hii ni hadithi ya kusisimua ya mapenzi kati ya Sam, anayetoka Kibera, makazi ya masikini kwenye jiji la Nairobi, Kenya, na Alissa, anayetoka Minnesota, Marekani: Bila shaka, hii ni hadithi ya mapenzi isiyo na kifani mwaka huu!!! Alissa anatoka Minnesota, huko Sam alizaliwa na kulelewa Kibera. Ilikuwaje ‘njiwa hawa wa...
Urabuni: Hijab na Ubaguzi wa Kimagharibi
Mwanablogu wa Mirsi Nadia El Awady anaandika posti ya blogu yake ambapo anahoji kama wanawake wanaovaa Hijabu wanabaduliwa kwenye nchi za magharibi ama la. Nadia, kama Mmisri alikulia Marekani na ameishi kwa kipindi kirefu Ulaya, anaelezea uzoefu wake kuhusu mwitikio alioupata kwenye nchi za Mashariki na Magharibi linapokuja suala la...
“Si rahisi kuwa Mhindi” nchini Marekani
Ricey Wild, Mmarekani wa asili anayeblogu kwenye blogu ya Indian Country Today, anandika kuhusu kuuawa kwa mbwa mwitu kwenye jimbo la Minnesota, Marekani. […]Rafiki yangu mpenzi Melissa alikuja kunichukua mwezi uliopita kwenda kwenye mkutano wa kupinga uwindaji wa mbwa mwitu kwenye jimbo la Mennesota na kwingineko. Tulipanda kaskazini na kuungana...
Rais Obama Kuitembelea Tanzania
Rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Afrika, Barack Obama anatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam kesho alasiri kwa ziara ya kiserikali. Blogu ya Swahili Time imeweka ratiba ya ziara hiyo ya siku mbili. Issa Michuzi aliweka video inayomwonesha Rais Kikwete wa Tanzania akizungumzia ziara hiyo.
Je, Una Swali Lolote kwa Jimmy Carter?
Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter anapokea maswali kupitia mitandao ya kijamii ya Facebook na Twita (#CarterQA) kama sehemu ya kuadhimisha miaka 30 ya Kituo cha Carter (Carter Center) kinachojishughulisha na “kupigania masuala ya amani na kupambana na magonjwa duniani kote”. Rais Carter atakuwa anayajibu maswali hayo kwa njia...
Marekani: Kumbukumbu la Walters Art lachapisha Mkusanyiko wa Picha
Jumba la Kumbukumbu la The Walters Art lililoko Baltimore, Maryland limechapisha zaidi ya picha elfu kumi na tisa kwenye mkusanyiko wa Wikimedia Commons na kuziweka chini ya leseni Creative-Commons. Jumba lenyewe lina mkusanyiko wa michoro kutoka Roma na Ulaya.
Urusi: Habari ya Putin-Berlusconi Kwenye WikiLeaks
Kwenye The Daily Beast, Julia Ioffe anatoa maoni juu ya masuala yaliyowekwa wazi katika Wikileaks kuhusu uhusiano kati ya Waziri Mkuu wa Urusi na mwenzake wa Italia Silvio Berlusconi.